Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ali Juma Shamhuna akiongoza
wahadhiri na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sumait Chukwani kuingia
katika kiwanja cha Mhafali. Wa kwanza (kulia) kaimu Makamu Mkuu wa chuo
hicho Prof. Hamad Rashid Hikmany (kushoto) Mwenyekiti wa Baraza la chuo
Dkt. Abdulrahman Al Muhailan. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ali Juma Shamhuna akiwahutubia
wanafunzi na wageni waalikwa katika mahafali ya 14 ya chuo Kikuu cha
Sumit Chukwani. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
Baadhi
ya wageni waalikwa wa mahafali ya 14 ya chuo Kikuu cha Sumait
wakifuatilia sherehe hizo zilizofanyika Chukwani Wilaya ya Magharibi
Unguja.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
……………………………………………………………………..
Na Miza Othman- Maelezo Zanzibar
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Amali Zanzibar Ali Juma Shamuhuna amewashauri wahitimu wa vyuo vikuu
nchini kutumia elimu na ujuzi wanaopata kujiajiri wenyewe badala ya
kusubiri ajira Serikalini.
Hayo aliyasema Chuo Kikuu cha
Abrahaman Al-Sumaait Memorial Chukwani (Sumait University) wakati wa
kuwatunuku shahada ya uwalimu wanafunzi waliohitimu mafunzo hayo
katika mahafali ya 14 ya chuo hicho.
Amesema kumekuwa na upungufu
mkumbwa wa ajira Serikalini, huku wahitimu wakiendelea kuongeza kila
mwaka. hivyo amewataka kutumia taaluma yao kujiajiri wenyewe na
kuisaidia jami zao.
“Nnawakumbusha kwamba kuna baadhi
ya taaluma soko lake la ajira limepungua, hivyo msikae kusubiri ajira
Serikalini bali itumieni elimu na ujuzi wenu ili kujitengezea ajira”,
Alisisitiza Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali..
Waziri Shamhuna ameupongeza
uongozi wa chuo hicho kwa kukipanua na kukipa hadhi zaidi kutoka Chuo
cha Elimu na sasa kuwa chuo Kikuu kamili na kupewa jina jipya la Sumait
University.
Alisema anaamini kazi hiyo haikuwa
rahisi kwa uongozi na wafanyakazi kuitekeleza bali ni matokeo ya kazi
ngumu na ushirikiano uliokuwepo kwa kipindi cha miaka mitatu ya
mageuzi hayo.
Katika kukiimarisha Chuo Kikuu cha
Sumait Waziri Shamhuna ameshauri kuongezwa fani za utafiti na masuala
ya ushauri ili kukipa hadhi zaidi na kutoa wanafunzi waliobora.
Aidha aliutaka uongozi wa Chuo
hicho kutafuta njia mbadala za kukiendesha badala ya kutegemea zaidi
malipo ya wanafunzi na misaada ya wahisani.
Akimkaribisha mgeni rasmi kutunuku
shahada kwa wahitimu, Mwenyekiti wa Baraza Kuu la chuo Dkt. Abdulrahman
Al-Muhailan alimpongeza Kaimu Makamu Mkuu wa chuo hicho Professa Hamad
Rashid Hikmany na wasaidizi wake kwa kazi kubwa waliofanya katika
kukifanyia mageuzi chuo hicho..
Aliishukuru Serikali ya Muungano
wa Tanzania kupitia Kamisheni ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kwa
ushauri na maelekezo mazuri waliowapa na hatimae kupata usajili katika
Kamisheni hiyo.
Alisema sera za chuo hicho katika
kipibndi cha miaka mitano inayomalizika mwaka 2017 ni kuwekeza miradi
ambayo itaingiza mapato na tayari wameanzisha jingo la ofisi itakayokuwa
na ehemu ya kutoa huduma kwa wageni mjini Dar es salaam.
Ameongeza kuwa hivi sasa
wanaimarisha Idara ya Uchapaji ya chuo hicho na kuiendesha kibiashara
ili kuwavutia wateja kutoka taasisi za umma na binafsi.
Jumla ya wahitimu 266
walikabidhiwa shahda zao katika mahafali hiyo na kufikisha idadi ya
wahitimu 1704 tokea kuanzishwa mwaka 1998.
No comments:
Post a Comment