Meneja
Mauzo wa StarTimes Tanzania, David Kisaka (kushoto) akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani), Dar es Salaam leo asubuhi wakati
wa uzinduzi wa bei mpya ya king’amuzi kitakakochouzwa kwa sh. 4000
sambamba na kifurushi kipya cha Nyota cha malipo ya sh. 4000 kwa mwezi,
Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa StarTimes Tanzania, Jacky Yu.
Bei hiyo mpya ya king’amuzi na kifurushi itamfanya mteja afurahie
chaneli zisizopungua 16 ikiwa 9 ni za kimataifa na 7 za nyumbani kwa
muda wa miezi saba na nusu.
Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa StarTimes Tanzania, Jacky Yu (kulia), akizungumza katika uzinduzi huo.
Baadhi ya wateja wakiangalia chaneli mbalimbali zinazorushwa na StarTimes kupitia vifurushi vyao mbalimbali.
…………………………………………………………………………………
KAMPUNI
ya StarTimes Tanzania ambayo inatoa huduma bora na nafuu za matangazo ya
digitali imezidi kupanua huduma zake baada ya kuja na kifurushi kipya na bei mpya ya king’amuzi kwa sh. 4000/- tu gharama ambayo ni ya chini kabisa kutowahi kutokea nchini.
Akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu huduma
hiyo mpya Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Kampuni ya Star Media
Tanzania ambao ni wauzaji wa ving’amuzi vya StarTimes nchini, Jacky Yu
amebainisha kuwa uzinduzi huo ni sehemu ya kutimiza ahadi kwa watanzania
kwamba watakuwa wakitoa huduma bora na kwa bei nafuu ambayo kila mtu
ataweza kuimudu.
“Leo
tunayo furaha kubwa kabisa kuwatangazia umma wa watanzania kwamba
StarTimes imeshusha bei ya king’amuzi chake mpaka kufikia sh. 4000 na
kuzindua kifurushi kipya na cha bei ya chini kinachokwenda kwa jina la
NYOTA ambacho kitapatikana kwa malipo ya sh. 4000 kila mwezi.”
“Kifurushi
hiki kipya cha NYOTA kina jumla ya chaneli zisizopungua 16, saba ni za
nyumbani na 9 ni za kimataifa ambazo ni Star Swahili, Bollywood Swahili,
E-Star, Star Music, Kungfu 1, Child Smile, TBN, TV Imani na CCTV News.
Ili mteja aweze kuunganishwa na kifurushi hiki itabidi aambatanishe na
malipo ya awali ya shilingi 30,000 na kuweza kufaidi kwa muda wa miezi
saba na nusu.” Alifafanua zaidi, Yu
Yu
alisema kuwa, baada ya muda wa ofa iliyotolewa kwa wateja wa kifurushi
kipya cha NYOTA kuisha, mteja ataamua kama anaendelea na kifurushi hiki
cha kulipia sh. 4000 kila mwezi au kutazama vingine vya kawaida. Ili
mteja kurudishwa katika vifurushi vya kawaida ambavyo vitamruhusu
kutazama chaneli za bure za nyumbani na kulipia vifurushi vilivyopo basi
itambidi afuate njia ya kawaida ya kujiunga ambayo ni rahisi kwa kupiga
*150*63# na kufuata maelekezo au atembelee ofisi zetu na za mawakala.
“Madhumuni
makubwa ya bei hii mpya ya king’amuzi na kifurushi cha NYOTA ni kumtaka
kila mtanzania hata Yule wa kipato cha chini aweze kupata matangazo ya
dijitali. Tuna imani kubwa kwamba kifurushi hiki kipya kitakidhi
mahitaji ya wateja wetu wote ambao wanapenda huduma zetu lakini
hushindwa kulipia gharama za vifurushi vilivyopo.” Alisema Bw. Yu na
kumalizia, “Siku zote StarTimes tutaendelea na dhamira yetu ya kutoa
huduma za uhakika na kwa bei nafuu ili kumfikia kila mteja. Tunaimani
matangazo ya dijitali ni fursa ambayo kila mtanzania lazima anufaike
nayo.”
Kwa
upande wake Meneja Masoko wa kampuni hiyo, David Kisaka aliongezea kwa
kusema, “kifurushi hiki kipya kimeongezewa katika vifurushi vyetu
vilivyopo, hivyo basi kuanzia leo hii tutakuwa na jumla ya vifurushi
vinne ambavyo ni NYOTA, Mambo, Uhuru na Kili. Tulichoongezea ni unafuu
na kuwajali wateja wetu kwani tunatofautiana kwa hali za kiuchumi na
tunafahamu kwamba watanzania wengi ambao ni wateja wanavipato vya
kawaida. Tunaamini kwa kifurushi hiki kipya cha NYOTA sasa tutawafikia
watanzania wote na kuwawezesha kufurahia matangazo ya dijitali.”
“Ningependa
kutoa wito kwa wateja wetu kutembelea maduka yetu na ya mawakala wetu
popote yalipo ili kuweza kuhudumiwa au kupiga namba ya huduma ya wateja
ambayo ni 0764 700 800 ili kupata maelezo na ufafanuzi zaidi. Na pia
ningependa kuwatoa hofu huduma hii ni endelevu kwani ni mwanzo tu wa
maboresho ya huduma zetu kwani kuna mabo mazuri lukuki yapo njiani
yanakuja. Na kwa wale wasio wateja wetu basi huu ndio muda muafaka kwa
wao kuunganishwa na huduma zetu, wameshapitwa na mengi lakini hili si la
kuliacha lipite hivi hivi.” Alihitimisha Kisaka. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)
No comments:
Post a Comment