Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Cosmas Mwaifwani (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam, wakati akitoa taarifa kwa Umma kuhusu utaratibu wa manunuzi ndani ya bohari ya dawa. Kulia ni Mkurugenzi wa Manunuzi wa MSD, Heri Mchunga na Mwanasheria, Domonica Meena.
………………………………………………………………………………..
Idara ya Bohari ya Dawa (MSD) iliundwa kwa sheria ya Bunge Na. 13 ya mwaka 1993. Ni Idara inayojitegemea chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ambayo ilianzishwa ili kuunda, kudumisha na kusimamia mfumo ulio bora na wenye gharama nafuu wa ununuzi, uhifadhi na usambazaji dawa na vifaa-tiba, vitendanishi kwa ajili ya hospitali navituo vya kutolea huduma ya afya nchini
Takwimu zilizopo kwa sasa zinaonyesha kuwa zaidi ya asilimia Themanini (80%) ya mahitaji yote ya Dawa,Vifaa tiba, Vitendanishi nchini vinatoka nje ya nchi hivyo taratibu za manunuzi hufuata taratibu na miongozo ya ndani ya nchi na ya kimataifa.
Utaratibu wa uagizaji na uingizaji wa dawa ndani ya nchi huratibiwa na kusimamiwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), kuwa dawa yoyote kabla ya kuingizwa chini lazima iwe imesajiliwa na Mamlaka na hukaguliwa pindi inapogombolewa ili kuhakikisha ubora wake. Sambamba na ukaguzi huo pia Bohari inavyo vitengo vya Ukaguzi wa Ndani (Internal Audit) na Uthibiti Ubora (Quality Assurance) ili kujihakikishia zaidi kuwa taratibu za manunuzi zinazingatiwa pia dawa zinazonunuliwa zinakidhi viwango vilivyokwishawekwa.
Aidha taribu za manunuzi katika Bohari kama ilivyo taasisi nyingine yoyote ya Serikali husimamiwa na kuongozwa na sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2011 na
kanuni zake za mwaka 2013. Taratibu za manunuzi huanza pale ambapo kuna uhitaji wa dawa fulani kutoka katika vituo vya kutolea huduma ya afya nchini. Mahitaji ya dawa kutoka katika vituo vya kutolea huduma ya afya huenda sambamba na mgawo wa fedha kwa kila kituo husika. Bohari inayo Bodi
ya Zabuni (MSD Tender Board) kwa mujibu wa Sheria ya Manunuzi ya Umma yenye wajumbe ambao ni wafanyakazi katika Bohari wa ngazi za juu na wenye utaalamu tofauti. Bodi ya Manunuzi
ndiyo chombo cha juu chenye maamuzi ya manunuzi ndani ya Bohari hivyo manunuzi yote ndani ya Bohari husimamiwa na Bodi hii.
ndiyo chombo cha juu chenye maamuzi ya manunuzi ndani ya Bohari hivyo manunuzi yote ndani ya Bohari husimamiwa na Bodi hii.
Njia inayotumika katika manunuzi ya bidhaa ndani ya Bohari ni kwa kupitia zabuni za kimataifa na hii ni kutokana na ukweli kwamba zaidi ya asilimia 80 ya bidhaa hutoka nje ya nchi. Zabuni ya kimataifa iko wazi kwa kila mshitiri ndani na nje ya nchi bila kubagua nchi anayotoka. Kigezo cha kwanza kwa mshitiri kushiriki katika zabuni ni kuwa na bidhaa yake imesajiliwa nchini na mamlaka zinazohusika na kigezo hiki cha kusajili hakina kinga kwa mshitiri yoyote yule.
Utangazaji wa zabuni hufuata na kutumia njia na machapisho ya kitaifa na Kimataifa kupitia tovuti (webistes) za Bohari (www.msd.or.tz) na ya Mamlaka ya Manunuzi ya Umma (www.ppra.go.tz). Aidha tunatumia Magazeti ya kimataifa, na ya kitaifa katika lugha za Kiingereza na Kiswahili ili kuwafikia watu wote. Zabuni hufunguliwa hadharani kwenye siku ambayo ilitamkwa kwenye gazeti na washitiri au wawakilishi wao hualikwa kwenye zoezi hilo ili kujiridhisha kuwa vigezo mbalimbali ikiwapo bei iliyotamkwa na uwepo wa nyaraka muhimu vimefuatwa
Baada ya ufunguzi hufuata mchakato wa tathmini (evaluations) kwa kutumia wataalamu huru kulingana na zabuni husika, wakati mwingine wataalam hao hutoka nje ya Bohari kulingana na utaalam wao katika zabuni husika.
Baada ya mchakato wa tathmni hufuata zoezi la kuwapata washindi , zoezi ambalo hufanywa na Bodi ya zabuni. Washindi hupatikana kutokana na vigezo vilivyoweka na hupaswa kutimizwa. Washitiri wote hupewa mrejesho juu ya mchakato mzima jinsi ya zabuni ilivyokwenda na matokeo yake. Bohari hutumia mfumo uliowazi, haki na usawa katika manunuzi ili kuhakikisha kunakuwa na ushindani na thamani fedha kwenye mali ya umma.
Sheria ya Manunuzi ya Umma inalinda haki za mshindani yeyote yule ambaye baada ya kwisha mchakato anaweza kuwa na hisia kuwa Bohari ya Dawa haikumtendea haki kwani inamruhusu kukata rufaa kwenye Mamlaka ya ya Manunuzi ya Umma (PPRA) ambao huitisha nyaraka zote toka Bohari na kuzipitia na kisha huzitolea maamuzi.
Ili kuhakikisha uwazi na haki, Sheria ya manunuzi inatutaka tuchapishe katika vyombo vya habari matokeo ya washindi wa zabuni wote kila mwisho wa mwaka. Taarifa ya zabuni yamwaka wa fedha wa 2012/ 13 iliiyotolewa kwenye Mwananchi la tarehe 27/ 12/ 13 na la The Guardian la tarehe 31/ 12/ 13 nairudia hapa ili kuonyesha washindi wa zabuni hizo, thamani na nchi ambazo makampuni hayo yanatoka.
Namba ya Zabuni Aina ya Bidhaa Kampuni iliyoshinda Thamani Tarehe ya kutoa mkataba Nchi
PHARMACEUTICALS
IE-009/2012/2013/HQ/G/30/04 Supply of Pharmaceuticals Samiro Pharmacy $ 3,379,327 12/7/2013 Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/30/05 Supply of Pharmaceuticals Tata Africa Holdings Ltd $ 177,668 12/7/2013 Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/30/13 Supply of Pharmaceuticals Nirma Limited $ 1,214,951 12/7/2013 India
IE-009/2012/2013/HQ/G/30/07 Supply of Pharmaceuticals Novo Nordisk A/S $ 1,516,643 12/7/2013 Denmark
IE-009/2012/2013/HQ/G/30/14 Supply of Pharmaceuticals Abacus Paraental Drugs Ltd $ 2,914,336 12/7/2013 Uganda
IE-009/2012/2013/HQ/G/30/03 Supply of Pharmaceuticals SG Star Pharmaceutical Limited Total $ 470,150 12/7/2013 Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/30/16 Supply of Pharmaceuticals Bahari Pharmacy Ltd Total $ 1,820,539 12/7/2013 Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/30/06 Supply of Pharmaceuticals Planet Pharmaceutical Ltd Total $ 846,730 12/7/2013 Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/30/08 Supply of Pharmaceuticals Serum Institute of India Total $ 953,577 12/7/2013 India
IE-009/2012/2013/HQ/G/30/10 Supply of Pharmaceuticals Medopharm PVT Ltd Total $ 386,009 12/7/2013 India
IE-009/2012/2013/HQ/G/30/09 Supply of Pharmaceuticals Pyramid Pharma Total $ 1,422,933 12/7/2013 Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/30/18 Supply of Pharmaceuticals Fresenius Kabi Total $ 1,294,587 12/7/2013 India
IE-009/2012/2013/HQ/G/30/01 Supply of Pharmaceuticals Jilichem (T) Ltd Total $ 6,473,661 12/7/2013 Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/30/04 Supply of Pharmaceuticals IDA Foundation Total $ 797,802 12/7/2013 Netherlands
IE-009/2012/2013/HQ/G/30/15 Supply of Pharmaceuticals Claris life sciences Limited Total $ 970,819 12/7/2013 India
IE-009/2012/2013/HQ/G/30/17 Supply of Pharmaceuticals Keko Pharmaceticals Industries (1997) Ltd Total $ 19,485,669 12/7/2013 Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/30/12 Supply of Pharmaceuticals Galentic Pharma (India) PVT Ltd Total $ 819,836 12/7/2013 India

No comments:
Post a Comment