Mbaji alisema jamii inapaswa kutambua kuwa watoto wenye ulemavu ni binadamu kama wengine na wanahaki sawa na wengine. “Kuna baadhi ya familia ambazo zimekuwa zikiwanyanyapaa watoto au watu wenye ulemavu kwa kuwalaza wakati mwingine kwenye vyumba vya mifugo kwa kweli huu ni unyama uliyopitiliza naviomba vyombo vya habari kwenda mbali katika majukumu yao kwa kuibua unyama huu hususan maeneo ya vijijini,”alisema Mbaji.
Mbaji alisema maeneo ya vijijini bado wazazi wanaendelea kuwakosesha mahitaji ya msingi watoto hao, ikiwemo elimu, wakidhani kuwa hawana uwezo wa kuelewa masuala mbalimbali watakayofundishwa. Alitoa wito kwa jamii kuwafichua watoto hao popote walipofichwa ili serikali iweze kuwapatia mahitaji yao kama wanayoyapata watu wengine wenye viungo kamili.
No comments:
Post a Comment