Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kulia)
akiwafafanulia jambo maafisa wa Wizara ya Mambo ya Ndani na Usalama ya
nchini Marekani katika mkutano wao uliofanyika jijini Washington DC
katika Ukumbi wa Mkutano wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani. Katika
mazungumzo yao maafisa hao wa Marekani wanatarajia kutua nchini Tanzania
kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa maafisa Uhamiaji, Polisi na Maafisa
Forodha ya kushirikiana kwa Serikali hizo mbili kwa ajili ya kudhibiti
mipaka kwa kuzuia bidhaa haramu zikwemo silaha, dawa za kulevya pamoja
na bidhaa mbalimbali za hatari kwa maendeleo ya nchi ambazo zinaweza
kuingizwa nchini kutoka kwenye nchi mbalimbali duniani. Waziri Chikawe
yupo nchini humo kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa
Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani hata hivyo alipata muda wa
kuzungumza na maafisa hao baada ya kuomba kukutana naye. Katikati ni
Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula. Picha
na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wanne kushoto),
Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula (watatu
kushoto), na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,
jijini New York, nchini Marekani, Tuvako Manongi wakiwa katika picha ya
pamoja na Maafisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani pamoja na
Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Ndani na Usalama ya nchini Marekani.
Waziri Chikawe alikutana na Maafisa hao wa Marekani, jijini Washington
DC kujadiliana masuala mbalimbali likiwemo la Maafisa hao wakitarajia
kuja nchini Tanzania kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa maafisa Uhamiaji,
Polisi na Maafisa Forodha ya kushirikiana kwa Serikali hizo mbili kwa
ajili ya kudhibiti mipaka kwa kuzuia bidhaa haramu zikwemo silaha, dawa
za kulevya pamoja na bidhaa mbalimbali za hatari kwa maendeleo ya nchi
ambazo zinaweza kuingizwa nchini kutoka kwenye nchi mbalimbali duniani.
Waziri Chikawe yupo jijini Washington DC katika Mkutano wa Kimataifa wa
Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani, hata hivyo alipata muda wa
kuzungumza na maafisa hao baada ya kuomba kukutana naye. Katikati ni
Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula. Picha
zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment