Balozi wa Japan nchini Tanzania
Mheshimiwa Masaki Okada akizumgumza na Mke wa Rais na Mwenyekiti wa
Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete pamoja na
uongozi wa Taasisi hiyo muda mfupi kabla ya kutiliana saini mkataba wa
mradi wa kupanua Shule ya Sekondari WAMA-Nakayama iliyoko Rufiji, Mkoani
Pwani tarehe 19.2.2015.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa
Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akitiliana
saini na Balozi wa Japan hapa nchini Mheshimiwa Masaki Okada kwenye
mradi wa upanuzi wa Shule ya Sekondari WAMA-Nakayama utakaogharimu dola
za kimarekani 498,738. Sherehe ya utiaji saini ilifanyika kwenye ofisi
za WAMA zilizopo karibu na Ikulu.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa
WAMA, Mama Salma Kikwete akibadilishana hati za Mkataba na Balozi wa
Japan hapa nchini Mheshimiwa Masaki Okada mara baada ya kutia saini zao
kwenye mkataba huo.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA
Mama Salma Kikwete akizungumza mara baada ya kumaliza kutiliana saini
mkataba wa mradi wa upanuzi wa Shule ya WAMA Nakayama.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA
Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Japan hapa
nchini Mheshimiwa Masaki Okada mara baada ya viongozi hao kutia saini
mkataba wa upanuzi wa Shule ya Sekondari WAMA-Nakayama.
PICHA NA JOHN LUKUWI
No comments:
Post a Comment