Kaimu
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Tigo, Cecile Tiano akizungumza katika
mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu mipango ya
kampuni hiyo kwa mwaka 2015 ambapo imepanga kuwekeza sh. bilioni 221
katika mtandao wake kwa mwaka 2015. Kulia ni Meneja Mawasiliano wa
Tigo, John Wanyancha.
Meneja Mawasiliano wa Tigo, John Wanyancha (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
………………………………
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI
ya simu ya Tigo Tanzania imepanga kutumia kiasi cha dola milioni 120
sawa na sh. bilioni 221 mwaka huu kwa ajili ya upanuzi wa mtandao wake
utakao ongeza ufanisi wa huduma zake nchini.
Hayo
yalibainishwa na Kaimu Meneja Mkuu wa Tigo, Cecile Tiano Dar es Salaam
leo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mipango ya
kampuni hiyo kwa mwaka 2015.
Tiano
alisema kwamba uwekezaji wa mwaka huu ni ishara ya nyongeza ya asilimia
20 kutoka dola milioni 100 za kimarekani (shilingi bilioni 184) ambazo
kampuni ilitumia katika kuboresha ufanisi wake kwa mwaka 2014.
“Ongezeko
hili la uwekezaji inadhihirisha nia yetu ya dhati katika kuwapatia
wateja wetu huduma bora ambazo zinapitiliza matarajio yao na kuwapa
Watanzania wengi zaidi uwezo wa kupata huduma ya mawasiliano nchini,”
alisema Tiano.
Akielezea
mwaka 2014 kama msimu mzuri, Meneja Mkuu huyo alisema kwamba Tigo
imeweka rekodi ya kukua kwa idadi yao ya wateja kutoka milioni saba na
kufika milioni 9 ambayo ni sawa na asilimia 30.
“Tunataka
kupanua na kuendeleza ubora wa mtandao wetu kwa kuwekeza katika minara
787 nchini kote. Baadhi ya minara hii itakua na uwezo wa intanet mwendo
kasi 4G na zingine 3G, ambayo ina maanisha kwamba maeneo ya vijijini
yatazidi kufikiwa zaidi pamoja na uwezo wa wateja wetu kutumia zaidi
vifurushi vya data,” alisema huku akitaja kwamba Tigo ina minara zaidi
ya 2,000 nchini kote.
Mipango
mengine kwa ajili ya 2015, kutokana na maelezo ya Tiano, ni ongezeko la
mara mbili ya idadi ya matawi ya huduma kwa wateja za Tigo kutoka 42
zilizopo sasa hadi 100 kwa ajili ya kuleta huduma za Tigo karibu zaidi
na wateja.
Ili
kuweza kuendeleza mabadiliko ya kidijitali nchini, Meneja huyo alisema
kwamba Tigo ina mpango wa kuzindua bidhaa na huduma zingine za kibunifu
mwaka huu kama ambavyo huduma ya ‘Tigo Music’ iliyozinduliwa hivi
karibuni imeweza kubadilisha tasnia nzima ya mziki kwa kuwapatia wateja
wa Tigo muziki ya kitaifa na kimataifa kupitia simu zao za mkononi.
Alisema
huduma ya kipekee ilitanguliwa na huduma zingine nyingi ambazo Tigo
ilikuwa kampuni ya kwanza ya simu kuzindua mwaka jana ikiwemo huduma ya
kutuma na kupokea fedha ya kimataifa yenye uwezo wa kubadilisha aina ya
Ankara moja kwa moja kwenye simu, huduma ingine ni Facebook ya Bure kwa
lugha ya Kiswahili.
Aliongeza
kuwa Tigo ndani ya mwaka 2014 pia iliunganisha huduma zake za kutuma na
kupokea fedha na benki kubwa zinazoongoza nchini ili kuwawezesha wateja
kuweka na kutoa fedha kutoka katika akaunti zao za benki kupitia
akaunti za simu za Tigo Pesa.
Alisema
muundo wa aina hiyo wa ushirikiano pia ulianzishwa na Tigo Pesa ili
kuweza kutuma na kupokea fedha kwa namna rahisi zaidi kwenda mitandao
mingine.
Alisema
Tigo itaendelea kutoa msaada mbali mbali ya maendeleo kwa jamii
kupitia mpango wake wa uwajibikaji kwa jamii ya mwaka 2015 ambayo
itajumuisha sekta ya elimu, afya, huduma za wanawake na watoto.
Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com
No comments:
Post a Comment