Waziri wa Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvu akiwa na ujumbe
watendaji wa NHC na Wizara yake amezuru Singapore na kutembelea Bodi ya
Maendeleo ya Nyumba na Wizara ya Mambo ya Nje kuvutia uwekezaji
Tanzania. Picha kamili na Muungano Saguya – SingaporeUjumbe
wa Tanzania chini ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
ukionyesha namna Serikali ya Singapore inavyoratibu upatikanaji wa
nyumba kwa wananchi wake ulipotembelea Bodi ya Maendeleo ya Nyumba ya
Singapore jana.Jumla ya nyumba 900,000 zimeshajengwa na Bodi hii na
kupatiwa wananchi kupitia ruzuku ya serikali na nyumba 50,000
zinapangishwa kwa wananchi kwa kodi isiyozidi asilimia 5. Taifa la
Singapore lina watu milioni 5.4 na asilimia 99 ya watu wan chi hiyo
wamewezeshwa kumiliki nyumba.
Ujumbe
wa Tanzania ukitembelea vyumba vya mfano vya ukubwa tofauti
vinavyojengwa na Bodi ya nyumba ya Singapore kwa ajili ya kuuzia au
kupangisha wananchi kulingana na uwezo, mahitaji na ukubwa wa familia.
Vyumba hivi vipo Makao Makuu ya Bodi ya Nyumba ya Singapore ambavyo ni
kivutio kwa wageni wanaotembelea jengo hilo kujifunza namna ya kuhudumia
watu wa kada mbalimbali wanaohitaji nyumba.
Ujumbe
wa Tanzania ukielezwa historia ya hatua mbalimbali za maendeleo ya
sekta ya nyumba nchini Singapore walipotembelea Bodi ya Maendeleo ya
nyumba nchini humo jana.
Ujumbe
wa Waziri Lukuvi ukiwa katika mji wa kisasa wa Punggol wenye ukubwa wa
kilomita za mraba kumi ambao una nyumba zilizojengwa na Bodi ya
Maendeleo ya Nyumba Singapore kwa ajili ya wananchi wa kipato cha kati
na chini. Katika eneo hili nyumba zimewekewa miundombinu ya kisasa na
zina watu wanaofikia 250,000. Hapa ni ghorofa ya pili ya jengo mojawapo
lililojengwa katika mji huu wa kisasa.
Mojawapo
wa majengo ya kisasa katika mji wa Punggol nchini Singapore
yanayokaliwa na wananchi waliouziwa na Bodi ya Nyumba ya Singapore
kupitia mifuko ya jamii na ruzuku ya serikali Ujumbe
wa Tanzania ukiwa eneo la Punggol Point Park ambalo ng’ambo yake ni
bandari ya nchi ya Malaysia inayopakana kwa karibu na nchi ya Singapore.
Ujumbe wa Waziri William Vangimembe Lukuvi ukiingia Wizara ya Mambo ya Nje ya Singapore ulipotembelea Wizara hiyo jana.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh.William Vangimembe Lukuvi
akiweka saini kwenye kitabu cha wageni muda mfupi baada ya kuingia
Wizara ya Mambo ya Nje ya Singapore. Kulia ni Naibu Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. Angela Kairuki.
Mh.
Waziri Lukuvi akisalimiana na Waziri wa Nchi Mwandamizi wa Mambo ya Nje
wa Singapore Bw. Masagos alipotembelea Wizara hiyo jana.
Ujumbe
wa Tanzania ukiwa katika mazungumzo na Waziri wa Nchi Mwandamizi Mambo
ya Nje wa Singapore. Katika mazungumzo hayo Tanzania imeiomba Serikali
ya Singapore kuwekeza nchini Tanzania hususan kwenye sekta ya nyumba,
kusaidia upangaji wa miji mikubwa na kuanzisha safari za ndege kuja
Tanzania ili kuvutia utalii. Nchi ya Singapore hupokea ndege 5800 kwa
wiki kutoka nchi mbalimbali duniani na ina zaidi ya ndege 200 zinazoenda
mataifa mbalimbali duniani hivyo kuwa kivutio kikubwa kuliko Tokyo
Japan.
Waziri
William Lukuvi akimpa zawadi ya kahawa na chai ya Tanzania, Waziri
Mwandamizi wa Nchi ya Singapore Bw. Masagos kama ishara ya kutangaza
bidhaa za Tanzania
Ujumbe
wa Tanzania ukiwa katika picha ya pamoja na Waziri Mwandamizi wa Mambo
ya Nje wa Singapore mara baada ya kumaliza ziara fupi ya kutembelea
Wizara hiyo jana kuvutia ushirikiano wa kiuchumi na nchi ya Singapore.
Ujumbe
wa Tanzania ukipata maelezo ya jinsi Shirika la Mipango Miji nchini
Singapore la Surbana linavyokabiliana na uhaba wa ardhi katika nchi
hiyo. Katika maelezo yake Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo Bw. Pang Yee Ean
alisema mipango ya ardhi ya Singapore huhuishwa kila baada ya miaka
mitano ili iendane na hali ya uchumi na mahitaji na kuna nidhamu ya hali
ya juu katika upangaji na matumizi ya ardhi ya nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment