Katibu
Tawala wa Mkoa wa Mtwara, Alfred Luanda (aliyesimama), akiwasilisha
taarifa fupi ya hali ya mmomonyoko wa ardhi uliosababisha mazingira ya
hatari kwa Kiwanda cha kuchakata gesi asilia cha Maurel & Prom
Tanzania (M&P), kilichopo Mnazi Bay – Mtwara. Wanaosikiliza ni
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (wa tatu kutoka
Kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu (katikati), na baadhi
ya Maafisa wa Wizara ya Nishati na Madini walioongozana na Waziri.
Baadhi ya nyumba wanazoishi wafanyakazi wa Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (wa pili kutoka Kulia) akikagua nyumba za wafanyakazi wa Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara. Pamoja naye ni Msimamizi Mkuu wa Mradi wa Bomba la gesi, Mhandisi Kapuulya Musomba (Kushoto – sambamba na Waziri) na Mkuu wa Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Nishati na Madini, Badra Masoud (Kulia kwa Waziri.
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (wa pili kutoka Kulia) akikagua nyumba za wafanyakazi wa Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara. Pamoja naye ni Msimamizi Mkuu wa Mradi wa Bomba la gesi, Mhandisi Kapuulya Musomba (Kushoto – sambamba na Waziri) na Mkuu wa Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Nishati na Madini, Badra Masoud (Kulia kwa Waziri.
Msimamizi
Mkuu wa Mradi wa Bomba la gesi, Mhandisi Kapuulya Musomba (kushoto),
akifafanua jambo kwa Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene
(wa pili kutoka kushoto) wakati akikagua nyumba za wafanyakazi wa Mtambo
wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara.
Sehemu ya Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara.
Waziri
wa Nishati na Madini, George Simbachawene, akikagua sehemu ya Mtambo wa
kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara wakati wa ziara aliyoifanya
mwanzoni mwa wiki mkoani humo.
Matanki
ya kuhifadhia maji kwa ajili ya matumizi mbalimbali, yaliyopo katika
eneo la Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara. Katika
ziara yake mtamboni hapo, Waziri wa Nishati na Madini, George
Simbachawene aliagiza maji hayo yatumike pia kuwasaidia wananchi
wanaoishi maeneo jirani.
Waziri
wa Nishati na Madini, George Simbachawene (katikati) akiwa katika picha
ya pamoja na wafanyakazi wa Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba –
Mtwara wakati wa ziara yake Mtamboni hapo mwanzoni mwa wiki.
Baadhi
ya Wafanyakazi/Vibarua katika Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa
Madimba – Mtwara, wakiendelea na kazi wakati Waziri wa Nishati na
Madini, George Simbachawene alipofanya ziara kukagua maendeleo ya Mradi
huo mwanzoni mwa wiki. Baadhi
ya Wafanyakazi/Vibarua katika Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa
Madimba – Mtwara, wakiendelea na kazi wakati Waziri wa Nishati na
Madini, George Simbachawene alipofanya ziara kukagua maendeleo ya Mradi
huo mwanzoni mwa wiki.
Sehemu ya Mtambo wa kuchakata gesi wa Madimba mkoani Mtwara. Waziri
wa Nishati na Madini, George Simbachawene (kulia) akijadili jambo na
mmoja wa wasimamizi wa Mtambo wa kuchakata gesi wa Madimba – Mtwara,
wakati wa ziara yake mwanzoni mwa wiki kukagua maendeleo ya Mradi.
…………………………………………………………………..
* Aahidi umeme kwa wana-Msimbati
Na Veronica Simba
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene amefanya ziara
mkoani Lindi na Mtwara mwanzoni mwa wiki kukagua miradi mbalimbali iliyo
chini ya Wizara yake ambapo aliahidi huduma za umeme na maji kwa
wananchi mbalimbali.
Akiwa Madimba mkoani Mtwara, baada ya kupokea taarifa ya
maendeleo ya ujenzi wa mtambo wa kuchakata gesi, Waziri Simbachawene
alimwagiza Msimamizi Mkuu wa Mradi wa Bomba la gesi, Mhandisi Kapuulya
Musomba kutoa huduma ya maji safi kwa wananchi wanaozunguka maeneo hayo.
“Kutokana na taarifa yenu, mtakuwa na hifadhi ya maji ya kutosha
hapa. Pamoja na matumizi yenu mbalimbali, hakikisheni mnatoa huduma ya
maji kwa wananchi wanaozunguka mtambo,” alisema Waziri.
Vilevile, Waziri Simbachawene alitoa ahadi ya umeme kwa Kijiji
cha Luvula kilichoko Msimbati. Alisema Kijiji hicho na vingine 15
vilivyo jirani na Kiwanda cha kufua umeme cha Mnazibay, vitapatiwa umeme
kabla ya mwezi Oktoba mwaka huu.
“Tunaendelea na zoezi la kusambaza umeme nchi nzima. Lengo letu
ni kuhakikisha idadi ya watanzania wanaopata umeme inaongezeka zaidi na
zaidi ili kuwezesha lengo la nchi yetu kufikia uchumi wa kipato cha kati
ifikapo mwaka 2025 kama dira ya maendeleo inavyoonesha,” alisema.
Ziara hiyo ya Waziri Simbachawene, ni ya kwanza kwa Mikoa ya
Lindi na Mtwara tangu aliposhika wadhifa wa Uwaziri wa Nishati na
Madini, Januari mwaka huu.
No comments:
Post a Comment