Genge
la wezi wa kompyuta limefanikiwa kuiba takriban dola bilioni moja
kutoka kwenye akaunti za wateja wa mabenki 100 katika mataifa 30.
Kampuni
inayosimamia usalama wa programu ya kompyuta inayohakikisha data ya
wateja iko salama Kaspersky Lab imesema katika ripoti yake maalum.Ripoti hiyo inaelezea mbinu mpya ya wezi wa Kompyuta wanaotumia mbinu mpya ya kudakua nambari za akaunti za wateja za siri kabla ya kuingia na kupora pesa .
Kaspersky imesema kuwa wizi huo ulianza mwaka wa 2013 na bado unaendelea hata leo kwani mabenki yote yalioathirika hayana uwezo wa kuwazuia wezi hao .
Hadi kufikia sasa ripoti hiyo inadai kuwa takriban dola bilioni moja zimeporwa kutoka kwenye akaunti za wateza.
Genge hilo la wezi, lililoanzia shughuili yake nchini Urusi, Ukraine na pia Uchina ndilo linalolaumiwa kwa wizi huo.
Kampuni hiyo ya Kaspersky inasema inafanya juhudi za kuzima wizi huo kwa ushirikiano na polisi wa kimataifa Interpol na polisi wa bara ulya Europol .
Kwa mujibu wa ripoti hiyo mabenki katika mataifa 30 yakiwemo, Russia, Marekani , Ujerumani , Uchina, Ukraine na Canada yameathirika pakubwa.
No comments:
Post a Comment