Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Wanawake
Tanzania (Twiga Stars), Rogasian Kaijage ametangaza kikosi cha
wachezaji thelathini (30) kitakachoingia kambini siku ya jumapili
kujiandaa na mchezo wa kufuzu Mataifa Afrika dhidi ya Zambia mwezi Machi
mwaka huu.
Kaijage ametangaza program yake
ya mazoezi itakayochukua takribani wiki nne (4) ili kuhakikisha
wachezaji wanakua tayari kwa ajili ya mchezo huo utakaochezwa kati ya
Machi 21, 22 mwaka huu, huku akipanga kucheza mchezo mmoja wa kirafiki
kabla ya kuelekea Lusaka Zambia kwenye mchezo wa awali.
Twiga Stars ambayo itakua kambini
katika Hosteli za Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF zilizopo
Karume, imeingia moja kwa moja katika hatua ya pili kucheza na Zambia
kufuatia kuwa na matokeo mazuri katika msimamo wa viwango vya soka la
wanawake barani Afrika.
Wachezaji walioitwa ni, Asha
Rashid, Esther Chaburuma, Fatuma Bushiri, Fatuma Hassan, Fatuma
Mustapha, Fatuma Omari, Eto Mlenzi, Mwajuma Abdallah, Sofia mwasikili,
Zena Khamis, Mwanahamis Omar, Fatuma Khatibu, Fadhira Hamad, Anastazia
Anthony, Shelder Boniface.
Wengine ni Thereza Yonna, Happines
Hezron, Amina Ally, Donizia Daniel, Fatuma Issa, Vumilia Maarifa,
Maimuna Hamisi, Najiati Abbasi, Stumai Abdallah, Ziada Ramadhani, Zuwena
Aziz, Irene Joseph (Mfunzo – Zanzibar), Dawa Haji Vuai (JKU –
Zanzibar), Belina Julius na Amina Ramadhani.
No comments:
Post a Comment