Yanga yaitandika BDF XI FC ya Botswana 2-0 uwanja wa taifa
Mchezaji
wa timu ya Yanga akiwania mpira katikati ya wachezaji wa timu ya BDF XI
FC ya Botswana wakati wa mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika
uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na Yanga kuibuka
na ushindi wa magoli 2-0 yaliyofungwa na mchezaji Hamisi Tambwe katika
dakika ya kwanza ya mchezo na dakika ya 55 , timu hizo zitarudiana baada
ya wiki mbili nchini Botswana.(PICHA KWA HISANI YA OTHMAN MICHUZI) Mchrezaji Kevin Yondani wa Yanga akiwania mpira na chezaji wa BDF XI FC ya Botswana wakati wa mchezo huo. Baadhi ya mashabiki wa Yanga wakiwa katika mchezo huo. Mrisho Ngasa akiwania mpira katika mchezo huo. Mchezaji Mbuyi Twite akirusha mpira Shabiki wa Yanga Babu Ali Tumbo akifanya vitu vyake wakati timu yake ya Yanga ikicheza.
MKUU WA MKOA WA RUKWA ENG. STELLA MANYANYA AKABIDHI KATIBA PENDEKEZWA KWA WILAYA ZOTE MKOANI RUKWA
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya kulia akimkabidhi Katibu Tawala
Wilaya ya Kalambo Bi. Mapinduzi Severian Katiba pendekezwa leo tarehe 14
Februari 2015 kwa niaba ya wananchi wa Wilaya hiyo ambao watapata fursa
ya kuiona na kuisoma kwa ajili ya kuipigia kura ya maoni mwezi Aprili
mwaka huu.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akimuonyesha muimbaji wa kikundi
cha ngoma za asili ya Kanondo Katiba pendekezwa katika hafla fupi ya
kukabidhi Katiba hiyo iliyofanyika katika Wilaya ya Kalambo. \
\Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akimuonyesha Ndugu Mulele Mulenda
Mwanaukawa aliyeshiriki hafla hiyo fupi ya kukabidhi Katiba pendekezwa
kwa niaba ya Katibu wa Chadema wa Wilaya ya Kalambo sehemu
ya vifungu vya katiba pendekezwa ambavyo vipo na vilikuwepo kwenye
rasimu ya Katiba ya Jaji J. Warioba ambpo ni kinyume na inavyodaiwa na UKAWA kuwa vimechakachuliwa.
Sehemu ya washiriki wa hafla hiyo, Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza na wananchi wa Wilaya
ya Kalambo muda mfupi baada ya kukabidhi Katiba pendekezwa. Aliwataka
wananchi hao kujitokeza kwa wingi mwezi April kwa ajili ya kuipigia kura
katiba hiyo na kutopotoshwa kwa namna yeyote ile na watu wasioitakia
mema nchi yao. Alisema kuwa katiba hiyo ni nzuri kwani imegusa maslahi
ya watanzania wote na ustawi wa taifa kwa ujumla.
Baadhi ya wananchi wakionekana kujifunika na mwanvuli kufuatia mvua iliyokua ikinyesha mwishoni mwa hafla hiyo.
RAIS WA ZANZIBAR AKUTANA NA WIZARA YA HABARI,UTALII,UTAMADUNI NA MICHEZO
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akiongoza kikao siku moja cha Wizara ya Habari,Utamaduni,Utalii na Michezo kilichozungumzia utekelezaji mpango kazi wa Wizara ya hiyo kwa kipindi cha mwezi Julai-Disemba 2014 katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar jana,[Picha na Ikulu.]
Baadhi ya Watendaji wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Utalii na Michezo na Idara zake mbali mbali wakimsikiliza Waziri wa Wizara hiyo Said Ali Mbarouk (hayupo pichani) alipokuwa akitoa taarifa ya Wizara ya utekelezaji wa mpango kazi kwa kipindi cha mwezi Julai-Disemba 2014 katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar jana chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,
Waziri wa Habari,Utamaduni ,Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk alipokuwa akitoa taarifa ya Wizara ya utekelezaji wa mpango kazi kwa kipindi cha mwezi Julai-Disemba 2014 jana katika kikao maalum kilichofanyika katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) na Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi pia Katibu Mkuu Kiongozi Dk.Abduhamid Yahya Mzee (kulia)
AWAMU YA KWANZA YA UANDIKISHAJI YA WACHEZAJI KWA AJILI YA KUJIUNGA NA KITUO CHA MICHEZO CHA NSSF-REAL MADRID SPORTS ACADEMY WAANZA RASMI
Mkurugenzi
wa Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam, leo wakati wa uzinduzi wa mchakato wa
usajili wa
vijana walio chini ya umri wa miaka 14, watakaochujwa kusaka nafasi ya kujiunga
na kituo kipya cha michezo cha NSSF–Real Madrid Sports Academy.
vijana walio chini ya umri wa miaka 14, watakaochujwa kusaka nafasi ya kujiunga
na kituo kipya cha michezo cha NSSF–Real Madrid Sports Academy.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori (katikati) akibadilishana mawazo na Mwakilishi wa Klabu ya Real Madrid, Rayco Ghasia (kulia).
Mzee Augustino Mtauka akisaini fomu za usajili wa kituo
kipya cha mchezo wa soka kinachomilikiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya
Jamii (NSSF) kwa kushirikiana na klabu ya Real Madrid ya Hispania.. Mzee Mtauka
alikuwa akisaini fomu hizo kwa niaba ya mjukuu wake Godfrey Oscar (katikati),
usajili uliofanyika kwenye Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam Jumamosi. Kulia ni Msajili Ally
Salehe wa Idara ya Elimu ya Michezo ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
kipya cha mchezo wa soka kinachomilikiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya
Jamii (NSSF) kwa kushirikiana na klabu ya Real Madrid ya Hispania.. Mzee Mtauka
alikuwa akisaini fomu hizo kwa niaba ya mjukuu wake Godfrey Oscar (katikati),
usajili uliofanyika kwenye Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam Jumamosi. Kulia ni Msajili Ally
Salehe wa Idara ya Elimu ya Michezo ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Msajili wa Vijana katika Program ya NSSF-Real Madrid
Sports Academy, Rachel Kayuni (kulia), kutoka Idara ya Elimu ya Michezo ya Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), akitoa maelekez kwa baadhi ya wazazi na vijana
waliokuwa wakisajiliwa kujiunga na kituo hicho cha soka kilicho chini ya
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa kushirikiana na klabu ya Real
Madrid ya Hispania. Usajili huo ulifanyika kwenye Uwanja wa Karume.
Sports Academy, Rachel Kayuni (kulia), kutoka Idara ya Elimu ya Michezo ya Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), akitoa maelekez kwa baadhi ya wazazi na vijana
waliokuwa wakisajiliwa kujiunga na kituo hicho cha soka kilicho chini ya
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa kushirikiana na klabu ya Real
Madrid ya Hispania. Usajili huo ulifanyika kwenye Uwanja wa Karume.
Mtoto
Osama Rashid akijaza fomu maalum kwa ajili ya kujiunga na kituo cha
michezo cha NSSF-Real Madrid Academy. Kulia ni mama yake Tatu Ali
akishuhudia.
Baadhi ya wazazi wakiondoka katika uwanja wa Karume baada ya kuandikisha watoto wao.
Badhi ya wazazi wakiwasimamia watoto wao katika zoezi la kujaza fomu kwa ajili ya kujiunga na kituo kipya cha michezo cha NSSF-Real Madrid Academy.
Mwakilishi
wa Klabu ya Real Madrid, Rayco Ghasia (wa pili kulia) akimsikiliza kwa
makini Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori (kushoto)
wakati wa uzinduzi wa zoezi la kuandikisha vijana watakaojiunga na kituo
kipya cha michezo.
Baadhi ya wadau wa soka wakiwa wameleta watoto wao kujisajili katika zoezi hilo.
Vijana
wakiingia katika uwanja wa Karume kwa ajili ya zoezi la kujisajili na
hatimaye kujiunga na kituo kipya cha michezo cha NSSF-Real Madrid
Academy.
Mwakilishi
wa FIFA katika masuala ya michezo hapa nchini, Henry Tandau (katikati)
akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa zoezi la kandikisha vijana
watakaojiunga na kituo kipya cha michezo cha NSSF-Real Madrid Academy.
Mtoto Issa Hashim akijaziwa fomu na Aisha Hashimu.
………………………………………………………………….
SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kwa
kushirikiana na Klabu ya Real Madrid ya Hispania, limezindua mchakato wa usajili wa
vijana walio chini ya umri wa miaka 14, watakaochujwa kusaka nafasi ya kujiunga
na NSSF–Real Madrid Sports Academy.
Mchakato huo wa usajili umefanyika leo kwenye Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam, ambako watoto kutoka Manispaa
za Ilala, Temeke na Kinondoni walisajiliwa na kuruhusiwa, zoezi linalotarajia
kuendelea leo.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo,
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori, aliwaka Watanzaia
kuwaleta vijana wao katika mchakato huo, na kwamba hakutakuwa na urasimu
utakaowakwamisha kusajiliwa.
Magori alisema kuwa, jukumu la kama NSSF ni kuratibu usajili
wa vijana wasiopungua 500, ambao watafanyiwa mchujo na Real Madrid kupata nyota
30 ambao wataingia rasmi katika darasa la kwanza kabisa la akademi hiyo
inayosubiriwa kwa hamu nchini.
“Wataalamu wanane wa lishe, tiba, afya na soka kutoka Madrid
watatua nchini wiki ijayo, kuwafanyia mchujo vijana wapatao 500 tunaotarajia
kuwasajili leo, kesho na wikiendi ijayo, ambao watafanya majaribio ya uwanjani
Februari 28,” alisema Magori.
Aliwataka wazazi na walezi wa watoto wenye vipaji,
kuhakikisha wanatumia fursa ya kuwafikisha watoto wao kwenye usajili, ili
kuwawezesha kupata nafasi ya kuwania kuingia miongoni mwa wakali 30 wa awali
watakaofungua darasa la akademi hiyo.
Alibainisha kuwa, kutokana na uharaka wa uanzishwaji wa
kituo, NSSF na Real Madrid hawatoweza kutembelea mikoani kufanya usajili kama
huo mwaka huu, badala yake akawataka wazazi wanaoweza kufika na watoto wao Dar
es Salaam kufanya hivyo.
Magori aliongeza kuwa, watoto watakaopata nafasi ya kuingia
katika akademi yao watasoma na kujifunza soka, ambapo watakaozivutia timu
mbalimbali barani Ulaya watauzwa na wale watakaokwama, watauzwa Afrika, ikiwamo
kuunda timu ya NSSF.
kushirikiana na Klabu ya Real Madrid ya Hispania, limezindua mchakato wa usajili wa
vijana walio chini ya umri wa miaka 14, watakaochujwa kusaka nafasi ya kujiunga
na NSSF–Real Madrid Sports Academy.
Mchakato huo wa usajili umefanyika leo kwenye Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam, ambako watoto kutoka Manispaa
za Ilala, Temeke na Kinondoni walisajiliwa na kuruhusiwa, zoezi linalotarajia
kuendelea leo.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo,
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori, aliwaka Watanzaia
kuwaleta vijana wao katika mchakato huo, na kwamba hakutakuwa na urasimu
utakaowakwamisha kusajiliwa.
Magori alisema kuwa, jukumu la kama NSSF ni kuratibu usajili
wa vijana wasiopungua 500, ambao watafanyiwa mchujo na Real Madrid kupata nyota
30 ambao wataingia rasmi katika darasa la kwanza kabisa la akademi hiyo
inayosubiriwa kwa hamu nchini.
“Wataalamu wanane wa lishe, tiba, afya na soka kutoka Madrid
watatua nchini wiki ijayo, kuwafanyia mchujo vijana wapatao 500 tunaotarajia
kuwasajili leo, kesho na wikiendi ijayo, ambao watafanya majaribio ya uwanjani
Februari 28,” alisema Magori.
Aliwataka wazazi na walezi wa watoto wenye vipaji,
kuhakikisha wanatumia fursa ya kuwafikisha watoto wao kwenye usajili, ili
kuwawezesha kupata nafasi ya kuwania kuingia miongoni mwa wakali 30 wa awali
watakaofungua darasa la akademi hiyo.
Alibainisha kuwa, kutokana na uharaka wa uanzishwaji wa
kituo, NSSF na Real Madrid hawatoweza kutembelea mikoani kufanya usajili kama
huo mwaka huu, badala yake akawataka wazazi wanaoweza kufika na watoto wao Dar
es Salaam kufanya hivyo.
Magori aliongeza kuwa, watoto watakaopata nafasi ya kuingia
katika akademi yao watasoma na kujifunza soka, ambapo watakaozivutia timu
mbalimbali barani Ulaya watauzwa na wale watakaokwama, watauzwa Afrika, ikiwamo
kuunda timu ya NSSF.
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHUDHURIA MISA MAALUM YA KUMUOMBEA MAREHEMU EVODIUS WALINGOZI KANISA LA MTAKATIFU JOSEPH DAR ILIYOONGOZWA NA MWADHAMA POLICARP KADINALI PENGO.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisaliamia na Mwadhama Policarp Kadinali Pengo, wakati wa Misa maalum
ya kumuombea Marehemu Evodius Walingozi, iliyofanyika leo Feb 14 kwenye
Kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam. Picha zote na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akijumuika na baadhi ya waumini wa dini ya Kikristu wakati wa Misa
maalum ya kumuombea Marehemu Evodius Walingozi, iliyofanyika leo Feb 14
kwenye Kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisaliamia na Mwenyekiti wa Bodi ya Madini Wizara ya Fedha Richard
Kasesela, wakati walipokutana katika Misa maalum ya kumuombea Marehemu
Evodius Walingozi, iliyofanyika leo Feb 14 kwenye Kanisa la Mtakatifu
Joseph jijini Dar es Salaam. Katikati yao ni Mwenyekiti wa Kanisa hilo,
Paul Mzuka.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiagana na Mwenyekiti wa Kanisla la Mtakatifu Joseph, Paul Mzuka,
baada ya kuhudhuria Misa maalum ya kumuombea Marehemu Evodius Walingozi,
iliyofanyika leo Feb 14 kwenye Kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es
Salaam.
COASTAL waitangazia vita Mbeya City.
NA MWANDISHI WETU,TANGA.
TIMU ya Coastal Union ya Tanga imesema kuwa itahakikisha inapambana vilivyo ili kuweza kuhakikisha inachukua pointi tatu muhimu dhidi ya Mbeya City kwenye mechi ya Ligi kuu soka Tanzania Bara itakayochezwa wikiendi hii kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani.
Coastal Union itangia kwenye mechi hiyo ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mechi yao ya mzunguko wa kwanza iliyochezwa kwenye uwanja wa sokoine jijini Mbeya ambapo Mbeya City iliweza kuibuka na ushindi wa bao 1-0 ambalo lilipatikana kwa njia ya penati.
Akizungumza maandalizi ya kuelekea mchezo huo,Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga alisema kuwa maandalizi ya kuelekea mechi hiyo imekamilika kwa asilimia kubwa kwa kufanya mazoezi asubuhi na jioni.
Amesema kuwa mipango yake mikubwa ni kuhakikisha wanafuta machungu ya kufungwa na Yanga bao 1-0, kwenye mechi yao ya Ligi kuu iliyochezwa kwenye uwanja wao wa nyumbani jambo ambalo halikuwafurahisha mashabiki na wapenzi wa soka.
Aidha amesema kutokana na kikosi chake kuendelea kuimarika kila mchezo wanaokuwa wakicheza wana matumaini makubwa ya kupata ushindi ambao utawawezesha kusogea kwenye nafasi za juu kwenye msimamo wa Ligi hiyo.
Alisema kuwa ligi kuu msimu huu imekuwa ni ngumu sana lakini kubwa ni kujipanga hivyo wamejipanga vizuri kwa umakini mkubwa lengo likiwa kukiwezesha kikosi hicho kinapata matokeo mazuri
TIMU ya Coastal Union ya Tanga imesema kuwa itahakikisha inapambana vilivyo ili kuweza kuhakikisha inachukua pointi tatu muhimu dhidi ya Mbeya City kwenye mechi ya Ligi kuu soka Tanzania Bara itakayochezwa wikiendi hii kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani.
Coastal Union itangia kwenye mechi hiyo ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mechi yao ya mzunguko wa kwanza iliyochezwa kwenye uwanja wa sokoine jijini Mbeya ambapo Mbeya City iliweza kuibuka na ushindi wa bao 1-0 ambalo lilipatikana kwa njia ya penati.
Akizungumza maandalizi ya kuelekea mchezo huo,Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga alisema kuwa maandalizi ya kuelekea mechi hiyo imekamilika kwa asilimia kubwa kwa kufanya mazoezi asubuhi na jioni.
Amesema kuwa mipango yake mikubwa ni kuhakikisha wanafuta machungu ya kufungwa na Yanga bao 1-0, kwenye mechi yao ya Ligi kuu iliyochezwa kwenye uwanja wao wa nyumbani jambo ambalo halikuwafurahisha mashabiki na wapenzi wa soka.
Aidha amesema kutokana na kikosi chake kuendelea kuimarika kila mchezo wanaokuwa wakicheza wana matumaini makubwa ya kupata ushindi ambao utawawezesha kusogea kwenye nafasi za juu kwenye msimamo wa Ligi hiyo.
Alisema kuwa ligi kuu msimu huu imekuwa ni ngumu sana lakini kubwa ni kujipanga hivyo wamejipanga vizuri kwa umakini mkubwa lengo likiwa kukiwezesha kikosi hicho kinapata matokeo mazuri
MAMA SALMA KIKWETE AWATAKA WANAWAKE WASISAHAU JUKUMU LAO LA MALEZI YA FAMILIA
Na Anna Nkinda – Maelezo, Lindi
14/2/2015 Wanawake kama wazazi wametakiwa kutimiza jukumu lao la malezi ya familia kwani wengi wao kutokana na hali halisi ya maisha wameacha kufanya kazi hiyo na kuwaachia wadada wa kazi.
Mwito huo umetolewa jana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia wilaya ya Lindi mjini Mama Salma Kikwete wakati akiongea na viongozi wa Halmashauri kuu ya tawi ya Chama hicho katika matawi ya Barabara ya Mchinga, Mitandi Magharibi na Kusini na Rutamba.
Mama Kikwete ambaye ni Mke wa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alisema kutokana na hali halisi ya maisha baadhi ya wamama wanamajukumu mengi ya kazi na jukumu la malezi ya watoto wamewaachia wa dada wa kazi jambo ambalo siyo zuri kwa makuzi ya mtoto.
“Tunajua kutokana na hali halisi ya maisha wanawake wengi wanahangaika kufanya kazi ili wapate fedha zitakazosaidia kuinua kipato cha familia lakini hata kama unamajukumu mengi jioni ikifika jitahidi ukae na familia yako mle pamoja chakula cha jioni kwa kufanya hivyo utajua matatizo yanayowakabili.
Imefikia hatua mama akimlisha chakula mtoto wake aliyemzaa yeye mwenyewe anakataa kula lakini akilishwa na dada wa kazi anakula na wamama wengine hata chai ya kunywa mmewe anatengewa na dada wa kazi badilikeni jamani”, alisisitiza Mama Kikwete.
MNEC huyo pia aliwasisitiza viongozi hao kupendana, kusaidiana na kufanya kazi kwa bidii na kujituma kwa kufanya hivyo watakuwa na maendeleo katika maisha yao na kuvisaidia vizazi vyao.
Akiwa katika tawi la Angaza mlezi huyo wa CCM wilaya ya Lindi mjini pia aliwahimiza viongozi hao kutoogopa kupima saratani za tezi dume na shingo ya kizazi kwani magonjwa hayo yakigundulika katika hatua ya awali yanatibika , mgonjwa anapona na kurudi katika hali yake ya kawaida.
Mama Kikwete alisema, “Kuna saratani ya tezi dume hii inawapata wanaume kuanzia umri wa miaka 45 na kuendelea. Kwa wanawake kuna saratani ya shingo ya kizazi, nawaomba msifanye masihara katika hili nendeni Hospitali mkapime kwani ukijua tatizo madaktari watatengeneza mazingira ya kutibiwa na kuliondoa tatizo hilo”.
Mama Kikwete yupo wilayani humo kwa ajili ya kuimarisha kazi za chama hicho ikiwa ni pamoja na kufanya vikao na viongozi na kuangalia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2010. Hadi sasa ameshatembelea matawi 78 kati ya 82 yaliyopo wilaya ya Lindi mjini.
SHIRIKA LA EQUALITY FOR GROWTH (EfG) LA ZINDUA MRADI WA MSAADA WA KISHERIA KWA WAFANYABIASHARA SOKONI NA OFISI ZAKE WILAYANI LUSHOTO MKOANI TANGA, FEBRUARY 13, 2015
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita akitoa hutuba fupi kwa mgeni rasmi.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Lushoto, Dk.Hassan Shelukindo akizungumza katika hafla hiyo.
Baadhi ya wasaidizi wa kisheria waliopatiwa mafunzo hayo.
Wanawake wa Wilaya ya Lushoto wakiwa kwenye sherehe hiyo ya uzinduzi wa mradi huo na ofisi.
Viongozi mbalimbali waliojumuika kwenye uzinduzi huo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita (mbele
katikati), akiwa katika picha ya pamoja na wasaidizi hao wa kisheria na
maofisa wa EfG.
Wanahabri
kutoka vyombo mbalimbali waliokuwepo kwenye uzinduzi huo. Kutoka
kushoto ni Shadrack (Channel 10), Nasra Abdallah (Tanzania Daima), Dotto
Mwaibale (Jambo Leo na Mtandao wa www.habari za jamii.com na Sophia kutoka Televisheni ya Mlimani.
Wanafunzi nao walijumuika kuona shughuli mbalimbali za uzinduzi huo hasa kikundi cha ngoma kilichokuwa kikitoa burudani.
Kikundi cha ngoma kikitoa burudani.
Zawadi zikitolewa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa EfG, Jane Magigita.
Mkurugenzi
Mtendaji wa EfG, Mary Magigita akiwa ameshika mkungu wa ndizi
aliozawadiwa. Kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Lushoto, Josephine
Kisigila.
Kaimu
Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Lushoto, Dk.Hassan Shelukindo
(kushoto), akifurahi na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality for
Growth (EfG), Jane Magigita baada ya kukabidhiwa machapisho mbalimbali
ya EfG.
………………………………………………………………………..
Doto Mwaibale
WAJASIRIAMALI
wanawake wametakiwa kutumia mafunzo ya usimamizi wa sheria katika
masoko waliyopata kwa kuwaelimisha wengine badala ya kukaa nyumbani bila
ya kutoa elimu hiyo.
Mwito
huo ulitolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Lushoto
Dk.Hassan Shelukindo wakati wa uzinduzi wa ofisi ya mradi wa msaada wa
kisheria kwa wafanyabiashara sokoni na ofisi ya mradi huo wilayani humo
mkoani Tanga jana kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmshauri hiyo Jumanne
Shauri.
“Ninyi
Wanawake wa Lushoto mmepata bahati kubwa ya kuletewa mradi huu pamoja
na mafunzo haya mliyopata nawaombeni nendeni mkayafanyie kazi katika
maeneo yenu” alisema Dk. Shelukindo
Alisema
elimu waliyoipata ya msaada wa kisheria ni muhimu sana kusaidia jamii
katika masoko na itasaidia kupunguza unyanyasaji wa kijisinsia.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth (EfG), ambalo linaendesha
mradi huo, Jane Magigita alisema lengo la mradi huo katika wilaya hiyo
ni kuhamasisha na kulinda haki za wafanyabiashara iwanawake katika
masoko kwa kuwapatia elimu ya sheria, biashara, elimu ya vicoba, elimu
ya uongozi na usimamizi wa vikundi.
Alisema
EfG ni shirika la pekee nchini linalotoa msaada wa kisheria kwa sekta
isiyorasmi hivyo kuonesha ni kiasi gani sekta hiyo ilivyo sahulika.
Alisema
EfG inaendesha mradi huo katika masoko ya wilaya ya Lushoto pamoja na
vikundi mbalimbali vya maendeleo na kuwa shirika hilo linawajibika kutoa
mafunzo ya siku 25 kwa wasaidizi 25 ambao watasambaza huduma sheria
kwa jamii.
Alisema mafunzo hayo yanatolewa kwa awamu tano ambapo kila awamu yatakuwa yanafanyika kwa takribani siku tano.
”
Shirika linawajibika kutoa mafunzo mafunzo mbalimbali kwa
wafanyabiashara ikiwa na lengo la kuinua hali za wanawake
wafanyabiashara sokoni kupitia mafunzo ya biashara, uundwaji wa vikundi
vya Vicoba, mafunzo mbalimbali kwa watendaji na viongozi wa Halmshauri
ya wilaya ya Lushoto kwa lengo la kuboresha hali za wafanyabiashara
sokoni” alisema Magigita.
Alisema
mpaka sasa shirika hilo limefanikiwa kuwapatia mafunzo ya sheria ya
siku tano wasaidizi wa sheria 25, wanaume 8 na wanawake 17 kutoka katika
masoko na wengine kutoka katika vikundi vya maendeleo ndani ya
Halmshauri ya Wilaya ya Lushoto.
Alisema
pia wanakituo maalumu cha msaada wa sheria katika ofisi za EfG Lushoto
ambapo wafanyabiashara mbalimbali wanaruhusiwa kupeleka matatizo yao ya
kisheria kila siku za Jumatatu na Jumatano kuanzia saa tatu asubuhi
mpaka saa 10 jioni.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)
NOEL OLE VAROYA CHADEMA ATANGAZA KUWANIA KITI CHA UBUNGE ARUSHA
Katika picha ni Noel Olevaroya
akihutubia Maelfu ya wananchi katika moja ya harakati zake katika
mkutano wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
…………………………………………………………………………
Aliyewahi kuwa mwenyekiti wa
vijana na mjumbe Wilaya ya Arusha kupitia chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA)Noel Olevaroya (37) ametangaza rasmi kupeperusha
bendera ya chama hicho kwa kuwania nafasi ya ubunge katika jimbo la
Arusha mjini.
Akizungumza na waandishi wa
habari jijini Arusha Noel Olevaroya alisema kuwa nia yake ya kugombea
nafasi ya ubunge katika jimbo la Arusha ni msukumumo kutoka kwa Mungu
baada ya kumaliza nafasi yake ya uwenyekiti wa vijana na mjumbe wilaya
ya Arusha mwaka 2014.
Alieleza kuwa msukumo huo
ulikuwa ukimsumbua sana na ndipo aliamua kutii sauti ya Mungu kwa
kutangaza kuwania nafasi hiyo ya kugombea kiti cha ubunge katika jimbo
la Arusha mjini ambapo kwasasa jimbo hilo lipo mikononi mwa Godbless
Lema.
Aidha alisema kuwa Mbunge
anafursa nzuri sana ya kusaidia wananchi hata kwa kupitia mfuko wa
jimbo,mshahara hali ambayo itasaidia kuwainua wananchi na kupunguza
umaskini.
Alitoa wito kwa vijana wa Arusha
kusikiliza sauti ya Mungu kwa kuwachagua viongozi bora wenye hofu ya
Mungu kwa maslahi ya Nchi yetu
(Habari na Pamela Mollel wa jamiiblog)
NAIBU WAZIRI WA MAJI AKAGUA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAJI SIHA
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akipanda mti katika ofisi za Bodi ya Udhamini ya Lawate Fuka Water Supply Trustee, katika Wilaya ya Siha, Mkoa wa Kilimanjaro ambayo inajiendesha yenyewe na mradi wake unahudumia vijiji 18, jumla ya wateja 3,318 wameunganishwa majumbani.
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla na Mkuu wa Wilaya ya Siha, Dk. Charles Mlingwa wakipata maelezo kutoka kwa Meneja Mradi wa Maji wa Bodi ya Udhamini ya Lawate Fuka Water Supply Trustee, Inj. Elihuruma Masaoe katika moja ya kituo cha maji kati ya vituo 290 vya mradi huo, Wilayani Siha, Mkoa wa Kilimanjaro.
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akikagua tenki la maji katika Kijiji cha Embukoi ambao ujenzi wake unaendelea, Wilaya ya Siha, Mkoa wa Kilimanjaro.
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla na Mkuu wa Wilaya ya Siha, Dk. Charles Mlingwa mara baada ya kukagua mradi wa Kijiji cha Makiwaru ambao unaendelea na ujenzi.
MKUU WA MKOA WA RUKWA AFUNGA MAFUNZO YA SIKU MBILI YALIYOANDALIWA NA TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA TANZANIA KWA KAMATI ZA MAADILI MIKOA YA RUKWA NA KATAVI LEO
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akisoma hotuba ya kufunga mafunzo
ya siku mbili yaliyoandaliwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama Tanzania
kwa kamati za maadili Mikoa ya Rukwa na Katavi na kufanyika Mjini
Sumbawanga tarehe 12-13 Februari 2015. Katika hotuba yake hiyo ameiomba
Serikali kutenga fedha ya kutosha ili mafunzo kama hayo yaweze kuwafikia
watu wengi zaidi kwa ustawi wa Sheria na Haki nchini. Mafunzo hayo ni
katika mkakati wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Tanzania kuimarisha tume za maadili nchini kusaidia maadili kwa watumishi wa Mahakama nchini. Kushoto ni Jaji Ferdinand Wambali muwezeshaji wa mafunzo hayo ambae ni Jaji wa Mahakama Kuu na Mkuu wa Chuo cha Mahakama Lushoto .
Bi Enzel Mtei ambae ni miongoni mwa wawezeshaji wa mafunzo hayo kutoka Tume
ya Mahakama Tanzania akimuwakilisha Mtendaji Mkuu wa Mahakama
akizungumza muda mfupi kabla ya kuhitimishwa mafunzo hayo. Miongoni mwa
maazimio yaliyofikiwa katika mafunzo hayo kwa wanakamati; Mihimili yote
ya dola nchini ifanye kazi kwa pamoja ili kutoa haki kwa wakati, Amri
halali itakayotolewa namamlaka husika iheshimiwe kuleta usawa wa
kisheria nchini na Mahakimu pamoja na wadau wengine wa sheria wawe mfano
kwa maadili bora katika jamii.
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa katikati na wajumbe wengine wakifuatilia mafunzo hayo.
Wajumbe wa Kamati ya maadili Mikoa ya Rukwa na Katavi wakifuatilia mafunzo hayo.
Wajumbe wa Kamati ya maadili Mikoa ya Rukwa na Katavi wakifuatilia mafunzo hayo.
Wajumbe wa Kamati ya maadili Mikoa ya Rukwa na Katavi wakifuatilia mafunzo hayo.
Wajumbe wa Kamati ya maadili Mikoa ya Rukwa na Katavi wakifuatilia mafunzo hayo.
Wajumbe wa Kamati ya maadili Mikoa ya Rukwa na Katavi wakifuatilia mafunzo hayo.
RAIS KIKWETE APOKEA UJUMBE KUTOKA KWA RAIS WA BURUNDI PIERRE NKURUNZINZA
.Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha ikulu mjumbe maalum wa Serikali
ya Burundi Sheikh Mohamed Rukara ambaye aliwasilisha ujumbe maalum
kutoka kwa Rais wa Burundi Pierre Nkurunzinza leo jioni.Sheikh Mohamed
Rukara ni Mkuu wa Utumishi katika serikali ya Burundi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribidhiwa ujumbe maalum Ikulu kutoka Serikali ya Burundi Sheikh Mohamed Rukara ambaye aliwasilishakutoka kwa Rais wa Burundi Pierre Nkurunzinza leo jioni.Sheikh Mohamed Rukara ni Mkuu wa Utumishi katika serikali ya Burundi
(picha na Freddy Maro)
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribidhiwa ujumbe maalum Ikulu kutoka Serikali ya Burundi Sheikh Mohamed Rukara ambaye aliwasilishakutoka kwa Rais wa Burundi Pierre Nkurunzinza leo jioni.Sheikh Mohamed Rukara ni Mkuu wa Utumishi katika serikali ya Burundi
(picha na Freddy Maro)
PSPF WATOA SEMINA KWA ASKARI NA WATUMISHI RAIA MAKAO MAKUU YA WIZARA YA MAMBO YA NDANI
Afisa
Matekelezo Mwandamizi(SCO) wa mfuko wa Pensheni wa PSPF Bi. Matilda A.
Nyallu akitoa elimu ya Mpango wa Uchangiaji wa Hiari kwa Askari na
watumishi raia makao makuu ya Wizara ya mambo ya ndani jijini Dar es
Salaam
Askari
na watumishi raia wakifuatilia elimu hiyo iliyokuwa inatolewa na
maafisa wa PSPF waliofika makao makuu ya Wizara ya mambo ya ndani kutoa
elimu ya Mpango wa Uchangiaji wa Hiari
………………………………………………………………………………………………..
Mfuko
wa penseni wa PSPF ulipata fursa ya kukutana na kutoa elimu kuhusu
huduma mbalimbali wanazo zitoa na kuweza kuwapa maelezo ya baadhi ya
mafao yanayo tolewa kupitia Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa (PSS) kwa Askari na watumishi raia makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani jijini Dae es Salaam.
Bi. Matilda A. Nyallu ambaye ni Afisa MatekelezoMwandamizi(SCO) wa mfuko wa PSPF aliweza kutoa rai kwa Askari na watumishi raia wote
waweze kujiunga na mfuko wa jamii wa PSPF ili kuweza kupata mafanikiona
kunufaika , Pia alitoa mifano michache kwa ambao watajiunga
na mfuko huo ambapo kwa Askari na watumishi raia alitaja
kuwa wanaweza kupata mikopo ya kuanzia maisha ambayo itakuwezesha
kupata nyumba ambazo wamezijenga kwa ajiri ya mtanzania aweze kununua au
kukopeshwa na baadae kuweza kurejesha mkopo huo wa nyumba, pia
aliongeza kwa kusema nyumba zote zimewekewa bima endapo tatizo lolote
likitokea basi nyumba hizo zitakuwa salama.
Hata
hivyo afisa wa mfuko wa Pensheni Bw.hadji Jamadary aliweza kuwaasa na
kuwasisitiza mambo mbalimbali yanoyo tekelezwa na mfuko na kuwataka wawe
miongoni mwa watu wenye muamko wa kujiunga ili wengine waweze kuiga
mfano kutoka kwao.
Mfuko wa pensheni ni mfuko wa kijamii unao toa huduma na kukidhi mahitaji ya jamii paspo na gharama zinazo iumiza jamii , kujiunga na mfuko wa PSPF ndiko kutakako kuokoa katika kukuwekea dhamana ya maisha yako iwe ni katika elimu ,makazi,ugonjwa na hata ujasiliamali
.
WAZIRI SIMBA AMSIMIKA CHIKAWE KUWA MLEZI UWT NACHINGWEA
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake
Tanzania (UWT), ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na
Watoto, Sophia Simba (kushoto) akimsimika kwa kumvalisha joho la ulezi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la
Nachingwea, mkoani Lindi, Mathias Chikawe, kuwa mlezi wa UWT katika
wilaya yake ya Nachingwea. Sherehe hiyo iliyohudhuriwa na mamia ya
wanachama wa UWT, ilifanyika katika Ukumbi wa NR mjini Nachingwea leo.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake
Tanzania (UWT), ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na
Watoto, Sophia Simba (kushoto) akimsimika kwa kumkabidhi fimbo ya ulezi
baada ya kumvalisha joho, kofia na skafu, Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, mkoani Lindi, Mathias
Chikawe, kuwa mlezi wa UWT katika wilaya yake ya Nachingwea. Sherehe
hiyo iliyohudhuriwa na mamia ya wanachama wa UWT, ilifanyika katika
Ukumbi wa NR mjini Nachingwea leo. Wapili kulia ni Mkuu wa wilaya hiyo,
Regina Chonjo, na wapili kushoto ni mwanachama wa UWT wilayani humo,
ambaye pia ni Mke wa Waziri Chikawe, Profesa Amandina Lyamba.
Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea,
Regina Chonjo (kushoto), Mke wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye
pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe, Profesa Amandina
Lyamba (kulia) wakilisakata rumba na wanachama wenzao wa Umoja wa
Wanawake (UWT) wilayani humo baada ya Mbunge wao kusimikwa rasmi na
Mwenyekiti wa UWT Taifa, ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii,
Jinsia na Watoto, Sophia Simba, kuwa mlezi wa UWT katika wilaya yake ya
Nachingwea. Sherehe hiyo iliyohudhuriwa na mamia ya wanachama wa UWT,
ilifanyika katika Ukumbi wa NR mjini Nachingwea leo.
Mlezi wa Umoja wa Wanawake (UWT)
Wilaya ya Nachingwea, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni
Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kushoto), akipokea
zawadi kutoka kwa mwakilishi wa UWT wilayani humo baada ya Waziri huyo
kusimikwa na rasmi na Mwenyekiti UWT Taifa, ambaye pia ni Waziri wa
Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba (kushoto kwa
Chikawe), kuwa mlezi wa UWT wilayani humo. Sherehe hiyo iliyohudhuriwa
na mamia ya wanachama wa UWT, ilifanyika katika Ukumbi wa NR mjini
Nachingwea leo.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake
Tanzania (UWT), ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na
Watoto, Sophia Simba akizungumza kwa furaha wakati akitoa hotuba yake
kwa wananchama wa UWT Wilaya ya Nachingwea baada ya kumsimika Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea,
Mathias Chikawe (kushoto) kuwa mlezi wa UWT wilayani humo. Sherehe hiyo
iliyohudhuriwa na mamia ya wanachama wa UWT, ilifanyika katika Ukumbi wa
NR mjini Nachingwea leo. Katika hotuba yake hiyo, Waziri Simba
alimuomba Waziri Chikawe aendelee kuisaidia UWT wilayani humo kama
alivyokuwa anafanya awali. Kulia ni Mwenyekiti wa UWT, Mkoa wa Lindi,
Faudhia Chiwangu.
Mlezi wa Umoja wa Wanawake (UWT)
Wilaya ya Nachingwea, ambaye pia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mathias Chikawe akiwashukuru wanachama wa UWT wilayani humo kwa
kumchagua kuwa mlezi wa umoja wao katika sherehe ya kusimikwa kwake
iliyofanyika mjini Nachingwea leo. Katika hotuba yake, Waziri Chikawe
ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, aliwaomba wanachama hao kuwa na
ushirikiano kwa kuijenga CCM, pamoja na kuhakikisha wanawahamasisha
wananchi jimboni humo kujiandikisha katika daftari la wapiga kura ili
kujiandaa kwa kuipigia kura Katiba iliyopendekezwa pamoja na Uchaguzi
Mkuu ujao. Kulia ni Mwenyekiti UWT Taifa, ambaye pia ni Waziri wa
Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba ambaye alimsimika
mlezi huyo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Regina Chonjo.
Mlezi wa Umoja wa Wanawake (UWT)
Wilaya ya Nachingwea, ambaye pia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mathias Chikawe (kulia), Mwenyekiti UWT Taifa, ambaye pia ni Waziri wa
Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba (katikati) na
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Nachingwea, Ng’ondomole Modesta Makota
wakiwaaga mamia ya wanachama wa UWT wilayani humo (hawapo pichani)
wakati walipokuwa wanatoka ukumbini. Waziri Chikawe alisimikwa na Waziri
Simba ili awe mlezi wa umoja huo na kuhakikisha kuwa UWT wilayani humo
inazidi kusonga mbele. Sherehe hiyo iliyohudhuriwa na mamia ya wanachama
wa UWT, ilifanyika katika Ukumbi wa NR mjini Nachingwea leo.
No comments:
Post a Comment