Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akikaribishwa na
Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula wakati
Waziri huyo alipowasili ubalozini hapo jijini Washington DC kujiandaa
kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani
unaotarajiwa kufanyika jijini humo kesho. Picha na Felix Mwagara, Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (katikati) akimsalimia
Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, jijini New
York, nchini Marekani, Tuvako Manongi wakati Waziri huyo alipowasili
ubalozi wa Tanzania nchini humo uliopo katika Jiji la Washington DC kwa
ajili ya kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi
duniani unaotarajiwa kufanyika jijini humo kesho. Kulia ni Balozi wa
Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula. Picha na Felix
Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Balozi
wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula (katikati)
akimtambulisha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (watatu
kulia) Maofisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini humo wakati Waziri huyo
alipowasili ofisini hapo, jijini Washington DC kwa ajili ya kushiriki
Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani
unaotarajiwa kufanyika jijini humo kesho. Picha na Felix Mwagara, Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wanne kulia) akizungumza na
Maofisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani baada ya Waziri huyo
kuwasili ubalozini hapo jijini Washington DC kwa ajili ya kushiriki
Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani
unaotarajiwa kufanyika jijini humo kesho. Katikati ni Balozi wa Tanzania
nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula. Picha na Felix Mwagara,
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (katikati), Balozi wa
Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula (kushoto) na
Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, jijini New
York, nchini humo, Tuvako Manongi wakiwa katika picha ya pamoja mara
baada ya kumpokea Waziri huyo aliyewasili jijini Washington DC kwa ajili
ya kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi
duniani unaotarajiwa kufanyika jijini humo kesho. Picha zote na Felix
Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment