Balozi wa Finland nchini Tanzania Bi. Sinnika Antilla.
==============================================
Na Abdulla Ali Maelezo-Zanzibar
Idara ya Ardhi na Mazingira inatarajia kufanya Uzinduzi wa Mfumo wa Mtandao wa Upatikanaji Taarifa za Ardhi
r (Zanzibar Land Information Service) (ZALIS) itakayosaidia upatikanaji wa taarifa sahihi za Ardhi nchini.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa
na Idara hiyo uzinduzi huo utafanyika siku ya Jumatano ya tarehe
18/02/2015 katika jengo la Ardhi liliopo Forodhani Mjini Zanzibar.
Kwa mujibu taarifa hiyo imesema
mtandao huo wenye teknolojia rahisi itakayosaidia kwa kiasi kikubwa
upatikanaji wa habari na taarifa zote za Ardhi ikiwemo usajili,
utambuzi, upimaji, uhaulishaji eneo, kijografia, mipaka na kuongeza
ufanisi wa shughuli zote ardhi kwa kiasi kikubwa.
Sambasamba na hayo taarifa hiyo
imeeleza kuwa mfumo wa ZALIS utarahisisha upatikanaji wa taarifa na
takwimu zinazohitajika Kijamii na Kiuchumi juu ya masuala ya Ardhi na
kuzifanya shughuli hizo kuwa rahisi na nyepesi zaidi.
Aidha Serikali ya Finland kupitia
Wizara yake ya Mambo ya Nchi za Nje imekuwa ikiisaidia Zanzibar katika
masuala mbalimbali ikiwemo Maji, Mazingira, Misitu pamoja na Ardhi kwa
zaidi ya miaka 10 hadi sasa.
Taarifa hiyo imefahamisha kuwa
Shughuli za usajili wa Ardhi zilizinduliwa rasmi mnamo mwaka 2013 na
Rais wa Zanzibar ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali
Mohamed Shein zikiwa zinaendelea vizuri nchini.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo
imeeleza maendeleo ya usajili wa Ardhi yamekuwa yakiendelea vizuri
nchini ambapo hadi sasa jumla ya vikataa 34,000 vimeshapatiwa usajili
wa kudumu Zanzibar.
Taarifa hiyo imesema hadi sasa
tayari kumeshaanzishwa Sera ya Taifa ya Ardhi, Mkakati wa Kitaifa wa
Maendeleo ya Matumizi ya Maeneo ya Ardhi, Mipango Kimkoa Kaskazini na
Kusini, Upitiaji wa Sheria zinazohusu Ardhi na Sera ya Mazingira na ile
ya Misitu zimeshafanyiwa mapitio na marekebisho.
Mfumo wa ZALIS umefadhiliwa na
Serikali ya Finland ambao umegharimu zaidi ya shilingi milioni 100
ambapo mgeni rasmi katika Uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Balozi wa
Finland nchini Tanzania Bi. Sinnika Antilla.
No comments:
Post a Comment