Kiungo
wa timu ya Coastal Union, John Mahundi amechaguliwa kuwa mchezaji bora
wa mwezi Disemba 2014 wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inayoendelea kutimua
vumbi kwenye viwanja mbalimbali nchini.
Mahundi alitoa mchango mkubwa kwa
timu yake ya Coastal Union mwezi Disemba mwaka jana na kuchaguliwa na
jopo la makocha linalofanya kazi ya kuchagua mchezaji bora wa kila
mwezi.
Aidha mshambuliaji wa timu ya
Polisi Morogoro, Said Bahanuzi amechaguliwa kuwa mchezaji bora mwezi
Januari 2015 wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inayoendelea kutimua vumbi
mzunguko wa 15 kwenye viwanja mbalimbali nchini.
Bahanuzi anayechezea timu ya
Polisi Morogoro kwa mkopo akitokea timu ya Young Africans amekua na
mchango mkubwa kwa timu yake tangu kujiunga nayo mzunguko wa pili wa
Ligi Kuu ya Vodacom nchini.
Kwa kuibuka wachezaji bora,
Mahundi na Bahanuzi watazawadiwa fedha taslimu sh. milioni moja kwa kila
mmoja kutoka kwa wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya simu za mkononi ya
Vodacom.
Jopo maalumu la makocha waliopo
katika viwanja vyote vinavyotumika kwa mechi za Ligi Kuu ya Vodacom
(VPL) ndiyo wanaofanya kazi ya kuchagua mchezaji bora kwa kila mechi kwa
kuzingatia vigezo vilivyowekwa, na baadaye alama zao kujumlishwa ili
kumpata mshindi wa mwezi.
No comments:
Post a Comment