Waziri wa Ujenzi Dkt. John
Magufuli kushoto akitoa maelezo kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal kuhusu Mzani
wa kisasa wa Vigwaza uliopo Mkoani Pwani ambao umekamilika kwa asilimia
99.8.
Mzani wa Kisasa wa Vigwaza kama
unavyoonekana. Mzani huu utapima magari kwa haraka zaidi kwa muda wa
sekunde 30 kwa kila gari tofauti na mizani ya sasa inayotumia dakika
moja na nusu mpaka mbili.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal akihutubia
wananchi katika Mzani wa Vigwaza mara baada ya kuukagua.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal akiwa na
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli pamoja na Mbunge wa Chalinze
Ridhiwani Kikwete, akikata utepe kuashiria ufunguzi wa barabara ya
Msoga-Msolwa km 10 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami.
Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt.
Mohamed Gharib Bilal akizungumza mara baada ya kutoa pole kwa wananchi
wa kijiji cha Msoga, Chalinze mkoani Pwani walioathirika na kimbunga
kikali kilichosababisha kubomoka kwa nyumba zaidi ya 40 katika kijiji
hicho pekee.
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani
Kikwete akicheza ngoma pamoja na kikundi cha ngoma cha Msoga
kusherehekea ufunguzi wa barabara ya Msoga-Msolwa yenye urefu wa km 10.
Barabara hiyo itapunguza msongamano wa magari katika eneo la Chalinze.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal akisalimiana
na watumishi wa TANROADS mara baada ya kukagua Mzani wa Vigwaza.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John
Magufuli kulia akisalimiana na Waziri wa Elimu ambaye pia ni Mbunge wa
Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa kabla ya ukaguzi wa Mzani wa Vigwaza.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Evarist
Ndikilo akiwa na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli wakielekea kwenda
kumpokea Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal katika eneo
la mzani wa Vigwaza mkoani Pwani. Picha zote kwa Hisani ya Kitengo cha
Mawasiliano Serikalini GCU-Wizara ya Ujenzi
No comments:
Post a Comment