Timu ya Taifa ya Tanzania ya Soka
la Ufukweni (Beach Soccer) kesho jumamosi itacheza mchezo wa marudiano
dhidi ya timu ya Taifa ya Kenya, mchezo utakaoanza majira ya saa 10
jioni kwenye Uwanja wa Escape One Club Msasani jijini Dar es salaam.
Wageni timu ya Taifa ya Soka la
Ufukweni kutoka nchini Kenya wanatarajia kuwasili leo jioni jijini Dar
es salaam, tayari kabisa kwa ajili ya mchezo huo wa marudiano siku ya
jumamosi na watafikia katika hoteli ya Saphire iliyopo eneo la Gerezani –
Kariakoo.
Katika mchezo wa awali uliofanyika
mwishoni mwa wiki jijini Mombasa, timu ya Taifa ya Tanzania iliweza
kuibuka na ushindi wa mabao 5 – 3 dhidi ya wenyeji timu ya Taifa ya
Kenya na kujitengenezea mazingira mazuri ya kusonga mbele katika hatua
inayofuata.
Waamuzi wa mchezo huo watakua ni ,
Beye Mbokh kutoka Senegal, mwamuzi wa pili ni Signate Youssouph
(Senegal), mwamuzi wa tatu, Maolidy Tsaralaza kutoka Madagascar, mtunza
muda (time keeper) atakua Hachim Said Nassur (Madagascar) na kamishina
wa mchezo atakua Roch Henriette kutoka Visiwa vya Shelisheli.
Tayari waamuzi wa mchezo huo
wameshawasili jijini Dar e salaam tangu jana jioni tayari kwa mchezo
huo, na endapo timu ya Taifa ya Tanzania itasonga mbele, itakutana na
timu ya Taifa ya Misri kati ya Machi 7, 8 na kurudiana kati ya Machi 13,
14, 2015.
Fainali za Soka la Ufukweni zinatarajiwa kufanayika mapema mwaka huu katika Visiwa vya Shelisheli.
No comments:
Post a Comment