Mshauri
mkuu wa mradi wa NewsRadar, Romana Gersuni kutoka Ujerumani akielezea
jinsi teknolojia hiyo mpya na ya kisasa ya ukusanyaji taarifa mbalimbali
ya Push Observer inavyofanyakazi zake.
mkuu
wa mikakati wa kampuni ya Six Telecoms ambayo ni kampuni mama ya Push
Observer, Rashid Shamte akielezea faida ambazo watazipata kampuni
mbalimbali nchini, husasani za kibiashara kwa kujiunga na huduma ya
NewsRadar waliyoianzisha nchii.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Push Mobile Fred Manento akizungumza na
waandishi wa habari kuhusiana na ufanisi wa mradi wa NewsRadar ambao
utawawezesha wafanyabiashara kupata taarifa mbalimbali kwa kutumia mradi
huo mpya na wa kisasa nchini
Afisa
Mawasiliano wa kampuni ya Push Observer, Tunu Makamula akiteta jambo na
wadau wa kampuni hiyo waliohudhuria semina elekezi na uzinduzi rasmi wa
mradi wa NewsRadar ambao utawawezesha wafanyabiashara kupata taarifa
mbalimbali kwa kutumia mradi huo mpya na wa kisasa nchini.
Sekta
zote Nchini sasa zinaweza kupata taarifa mbali mbali zilizorushwa kwene
vyombo vya habari kupitia teknolojia mpya ya usambazaji taarifa
ijulikanayo kwa jina la NewsRadar ya kampuni ya Push Observer.
zote Nchini sasa zinaweza kupata taarifa mbali mbali zilizorushwa kwene
vyombo vya habari kupitia teknolojia mpya ya usambazaji taarifa
ijulikanayo kwa jina la NewsRadar ya kampuni ya Push Observer.
Push
Observer Limited ni kampuni ya Tanzania inayomiliki vyombo vya
kiinteligencia na teknolojia ya sanaa ya kufuatilia, kukamata na kuchuja
vyombo vya habari – magazeti, matangazo (radio & televisheni),
Internet na uchambuzi, ripoti ya ushindani kwa ajili ya biashara,
serikali na wateja wengineo wa mashirika yasiyo ya kiserikali.
Hivi
sasa, Push Observer wanachunguza vituo vya redio 90+, vituo vya
televisheni 15+, magazeti (magazeti, majarida, magazeti na majarida) 70+
na machapisho online ikiwa ni pamoja na blogs na mitandao maudhui.
Observer ni kampuni ya kiTanzania inayoongoza kidigitali, kwa viwango
vya kimataifa na ushirikiano wa kimataifa katika data na uanachama na
vyombo kama FIBEP, Nudge, Vision Critical, na Harvard Innovation Labs.
Kwa
mujibu wa Mkuu wa Mikakati wa Six Telecoms, Kampuni mama ya Push
Observer, Rashid Shamte alisema kuwa kupitia teknologia hii ya
usambazaji ya kisasa, wateja wao wataweza kupata habari taarifa muhimu
na mpya masaa ishirini na nne ya wiki. Aliongeza kuwa,tumezindua
teknolojia hii kwa wateja wetu kutokana na teknologia ya uchunguzi wa
vyombo vya habari kubadilika sana miaka ya karibuni”.
“Huduma
hii ya kusambaza taarifa imekuwa ya kisasa, rahisi na ya ubora wa hali
ya juu kutokana na uwekezaji wetu katika teknolojia hii. Wana vifaa vya
kisasa ambavyo vinaweza kupata taarifa kupitia televisheni, magazeti,
mitandao ya kijamii na redio kwa muda muafaka, vifaa hivyo vinauwezo wa kupata taarifa had 350,000 kutoka vyombo mbali mbali. Kwa kutambua
mahitaji ya wateja wetu kupata habari na taarifa za muhimu tumeamua
kuzindua huduma hii na ili kuwahakikishia wateja wetu upatikanaji wa
taarifa muhimu na taarifa zinginezo za kwene vyombo vya habari kwa muda
muafaka” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Push Observer, Tom Kyalo.
No comments:
Post a Comment