Mchezo huo wa kirafiki ni sehemu
ya maandalizi ya timu hiyo kutoka nchini Zambia ambayo imeweka kambi
jijini Dar es salaam kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu
nchini Zambia.
Mara baada ya mchezo huo, Kikosi
cha Red Arrows kitaendelea na mazoezi kwenye uwanja wa Karume na Ufukwe
wa Mbalamwezi kulingana na ratiba ya kocha wa timu hiyo.
Red Arrows watacheza mchezo wao wa
pili na mwisho wa kirafiki siku ya jumapili dhidi ya timu ya Ruvu
Shooting inayoshiriki Ligi Kuu (VPL), mchezo ambao utachezwa kwenye
Uwanja wa Karume jijini Dar es salaam kabla ya kumaliza ziara yao siku
ya jumanne na kurejea nchini Zambia.
No comments:
Post a Comment