……………………………………………………………………………
Siku Ya Wanawake Dunia
huadhimishwa kila ifikapo Tarehe 8, mwezi wa tatu. Siku hii huadhimishwa
kwa shughuli mbalimbali na kutambua mchango wa mwanamke katika
maendeleo ya Jamii.
Mwaka huu kitaifa Siku hii
itaadhimishwa mkoani Morogoro lakini kampuni ya TruMark ya mjini Dar es
Salaam imeandaa warsha maalum katika maadhimisho hayo ambayo itafanyika
kwenye ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam Machi 7 mwaka huu.
Kauli mbiu ya Siku hii ni Women Make It Happen’ ikiwa inamaanisha wanawake wanafanikisha.
TruMark imeamua kufanya tamasha
hili, baada ya uzoefu tulioupata katika shughuli zetu za mafunzo ambazo
tunatoa kwa watu mbalimbali, tulioana kuna changamoto mbalimbali ambazo
wanawake wanazipata.
Hii likafanya tuone kuwa Siku Ya
Wanawake ni jukwaa ambalo linaweza kukutanisha wanawake katika kada
mbalimbali na kuzungumza mambo yao katika kujikwamua kiuchumi na
kujifunza kwa wengine ambao walipitia changamoto hizo lakini leo hii
wameweza kufika mbali baada ya kupambana.
TruMark imepata Baraka zote kutoka
Wizara ya Wanawake Jinsia na Watoto katika kuandaa siku hii muhimu.
Kwenye maadhimisho haya, kutakuwa na mada ambazo zitatolewa na wanawake
kutoka katika kada tofauti, juu ya uongozi, biashara na uchumi,
ujasiriamali.
Lakini pamoja na elimu ambayo
itatolewa kutakuwepo na burudani pia kutoka kwa wasanii wanawake maarufu
na chipukizi nchini ambao wataungana na wanawake wengine kusheherekea
siku yao hii.
Wanawake wanakaribishwa kushiriki
katika siku hii ili kuweza kupata elimu ambayo itawasaidia kwenye
shughuli zao za kila siku. Kwa upande mwingine tunatoa wito kwa
wadhamini kujitokeza ili kufanikisha siku hii kwani mama ndiye kiungo
cha familia.
No comments:
Post a Comment