Askari
mmoja wa jeshi la wananchi ameuawa kwa kupigwa risasi huku wengine
wanne wa jeshi la polisi wamejeruhiwa vibaya na kulazwa katika hospitali
ya rufaa ya mkoa wa tanga bombo kufuatia mashambilizi ya kurushiana
risasi katika mapango kati yao na vikundi vinavyodaiwa kuwa vya kigaidi.
Habari kutoka katika eneo la tukio zinadai kuwa vikundi hivyo
vilikuwa ndani ya mapango huku askari wakiwa nje hatua ambayo imedaiwa
kuwa majibizano ya risasi yalisababisha askari wa jeshi kupigwa ya
tumboni na kuwahishwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa tanga bombo
lakini baadae alifariki Dunia.
Baadhi ya wananchi waliozungumza na ITV wameingiwa na hofu kufuatia
tukio hilo huku baadhi yao wakidai kuwa wanashindwa kutoka katika
nyumba zao kwa kuhofia usalama wao kufuatia milio ya risasi katika eneo
la amboni hasa nyakati za usiku .
Hata hivyo kamishna wa Polisi -Operesheni na mafunzo Paul Changonja
akielezea tukio hilo amekiri kuwa askari wake watatu na mmoja wa jeshi
la wananchi wamejeruiwa kwa risasi wakati askari wake walipoingia katika
mapango hayo ndipo mmoja kati ya wanakikundi hao aliporusha risasi na
kuwajeruhi askari.
Hata hivyo jitihada za ITV kwenda katika eneo la tukio ziligonga
mwamba baada ya askari polisi wa kikundi cha (FFU) kuweka ulinzi na
kudai kuwa hatakiwi mwandishi wa habari kwenda katika eneo hilo huku
mganga mkuu wa mkoa wa tanga Dr,Asha Mahita naye akitoa maelezo kama
hayo kuwa waandishi wazuiwe wasiingie katika wodi ya galanosi kwa ajili
ya kuwaona askari waliojeruhiwa.
Jeshi la wananchi kwa kushirikiana na polisi nchini limeongeza askari
wa vikosi vya ardhini katika zoezi la kukabiliana na vikundi
vinavyodaiwa kuwa vya kigaidi katika mapango ya mleni yaliyopo eneo la
amboni jijini Tanga kufuatia askari wa jeshi la wananchi kuuawa kwa
risasi huku wengine wakijeruhiwa katika mapigano baina yao na vikundi
hivyo.
ITV imeshuhudia msafara wa magari ya kijeshi pamoja na yale ya
maofisa wa kijeshi na huduma ya kwanza yakipita katika barabara kuu
itokayo Tanga kwenda Horohoro mpakani mwa Kenya na Tanzania kisha
kuingia katika njia iendayo katika mapango yaliyodaiwa kuwa ni sehemu
maalum ya maficho ya vikundi hivyo vya kigaidi na msemaji wa polisi
kamishna wa polisi -operesheni Paul Chagonja kutwa nzima simu yake
iliita bila majibu lakini msaidizi wake alipoke na kudai kuwa bosi wake
yupo kwenye kikao.
Hata hivyo baadhi ya familia zilizopo katika eneo la Mleni
zinadaiwa kuhamisha makazi kufuatia milipuko ya risasi na silaha nzito
za kijeshi zilizokuwa zikirindima katika kipindi cha siku mbili nyakati
za mchana na usiku, hatua ambayo baadhi ya makundi ya vijana
yanaojihusisha na kazi ya kupasua mawe katika mapango hayo kulalamikia
ukosefu wa kazi kwa sababu ya mapigano hayo ambayo pia yamewapa hofu na
maisha yao.
Baadhi ya wakazi wa jiji la Tanga wameshauri mapango hayo
yaharibiwe kwa kutumia vifaa maalum vya kivita na jeshi la polisi
lisahau suala la silaha zao zilizoibwa katika matukio tofauti na makundi
hayo.
Via>>ITV
No comments:
Post a Comment