Serikali
ya Ugiriki imeleezea imani yake kwamba mkataba kuhusu madeni yake,
utafikiwa ndani ya saa arobaini na nane, licha ya kupinga muda wa mwisho
uliowekwa na nchi za Ulaya zinazotumia sarafu ya euro.
Mkutano wa
mawaziri kutoka nchi za Ulaya zinazotumia sarafu ya euro waliokutana
mjini Brussels, Ubalegiji ulivunjika mapema kuliko ulivyotarajiwa wakati
serikali ya Ugiriki kutupilia mbali fursa iliyotolewa kwa nchi hiyo
hadi Ijumaa kuhusu mpango wa nchi hiyo kudhaminiwa, au kuona mipango
ikiisha kufikia mwishoni mwa mwezi huu.
Vyanzo vya habari kutoka ndani ya serikali ya Ugiriki vinasema pendekezo la nchi za ulaya ni "upuuzi" na "halikubaliki".
Lakini
waziri wa fedha wa Ugiriki, Yanis Varoufakis, amesema Ulaya itafanya
"ulaghai uliozoeleka" kwa kutumia mkataba usio na ufumbuzi wa hali
iliyopo.
No comments:
Post a Comment