Chama cha kandanda mkoa wa Dar
es salaam DRFA,kimewapongeza wawakilishi wa Tanzania bara katika
michuano ya vilabu barani afrika klabu ya Azam FC na Yanga SC,kwa kuanza
na ushindi katika mechi zao za mkondo wa kwanza mwishoni mwa juma.
Yanga walikuwa wa kwanza kuwapa
raha watanzania siku ya jumamosi katika uwanjwa wa taifa jijini,baada ya
kuifunga mabao 2-0 timu ya maafande wa Polisi toka Botswana BDF
11,mabao yete hayo yakitupiwa nyavuni na mshambuliaji Amis Tambwe,ikiwa
ni mchezo wa kuwania kombe la shirikisho.
Kwa upande wa Azam FC,wao
waliwafunga wababe wa soka huko Sudan klabu ya El-Merekh kwa mabao 2-0
yaliyofungwa na Didier Kavumbagu pamoja na John Rafael Bocco,katika
mchezo wa kuwania kombe la klabu bingwa uliopigwa katika dimba la Azam
Cpmplex Chamazi.
Mwenyekiti wa DRFA,Almas
Kasongo,amewapongeza wawakilishi hao wa Tanzania kwa hatua hiyo nzuri
waliyoanza nayo,na kusema kuwa maandalizi yaliyofanywa na vilabu hivyo
kuelekea mashindano hayo ya afrika,pamoja na ubora wa wachezaji na
makocha,ni dhahiri kwamba vitafanikiwa kuvuka katika hatua hiyo ya
kwanza.
Kasongo,pia amesema DRFA
imeridhishwa na muitikio wa mashabiki wa Dar es salaam na maeneo mengine
nje ya jiji kwa kujitokeza kwa wingi kushuhudia mechi hizo mbili,na
kuwapongeza pia viongozi wa vilabu kwa matayarisho waliyoyafanya licha
ya dosari ndogo ndogo zilizojitokeza.
No comments:
Post a Comment