Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akimsikiliza kwa makini Rais
Barack Obama (hayupo pichani) wakati alipokuwa anatoa hotuba yake
katika Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani
uliofanyika katika Ukumbi wa Loy Henderson wa Wizara ya Mambo ya Nje,
jijini Washington DC nchini humo leo. Mkutano huo uliowashirikisha
Mawaziri wanaoshughulika na masuala ya usalama kutoka mataifa mbalimbali
duniani, Maafisa Waandamizi wa Umoja wa Mataifa (UN), Vyama vya Kiraia
na Sekta Binafsi ulijadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupambana na
vurugu na ugaidi dunaini. Katika hotuba yake, Obama alisema mapambano
dhidi ya watu wenye msimamo mkali hayawezi kulinganishwa na mapambano
dhidi ya waislamu, hivyo hakuna dini yoyote inayowajibika kwa ugaidi,
isipokuwa watu ndio wanaowajibika kwa vurugu na ugaidi. Picha zote na
Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Rais
wa Marekani, Barack Obama akitoa hotuba yake katika Mkutano wa
Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani uliofanyika katika
Ukumbi wa Loy Henderson, Wizara ya Mambo ya Nje, jijini Washington DC
nchini humo leo. Mkutano huo uliowashirikisha Mawaziri wanaoshughulika
na masuala ya usalama kutoka mataifa mbalimbali duniani, Maafisa
Waandamizi wa Umoja wa Mataifa (UN), Vyama vya Kiraia na Sekta Binafsi
ulijadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupambana na ugaidi pamoja na
vurugu mbalimbali dunaini. Katika hotuba yake, Obama alisema mapambano
dhidi ya watu wenye msimamo mkali hayawezi kulinganishwa na mapambano
dhidi ya waislamu. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe
aliiwakilisha Tanzania katika mkutano huo. Picha zote na Felix Mwagara,
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kushoto-mstari wa
pili), Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula
(nyuma ya waziri) wakimsikiliza kwa makini Rais Barack Obama (hayupo
pichani) wakati alipokuwa anatoa hotuba yake katika Mkutano wa Kimataifa
wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani uliofanyika katika Ukumbi wa
Loy Henderson wa Wizara ya Mambo ya Nje, jijini Washington DC nchini
humo leo. Mkutano huo uliowashirikisha Mawaziri wanaoshughulika na
masuala ya usalama kutoka mataifa mbalimbali duniani, Maafisa Waandamizi
wa Umoja wa Mataifa (UN), Vyama vya Kiraia na Sekta Binafsi ulijadili
masuala mbalimbali ya jinsi ya kupambana na vurugu na ugaidi dunaini.
Katika hotuba yake, Obama alisema mapambano dhidi ya watu wenye msimamo
mkali hayawezi kulinganishwa na mapambano dhidi ya waislamu, hivyo
hakuna dini yoyote inayowajibika kwa ugaidi, isipokuwa watu ndio
wanaowajibika kwa vurugu na ugaidi. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment