Mkuu
wa mkoa wa Njombe kapteni Mstaafu Aseri Msangi(katikati) akikagua
majengo ya shule mpya wa wasichana wilayani Makete, kushoto ni mkuu wa
wilaya ya Makete Josephine Matiro na kulia ni mwenyekiti wa halmashauri
ya wilaya ya Makete Daniel Okoka.
Ukaguzi huo ukiendelea.
Wananchi wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Njombe Kapteni Msangi(hayupo pichani) akizungumza nao
Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro akizungumza kwenye mkutano shuleni hapo
Mkuu wa mkoa wa Njombe Kapteni Mstaafu Aseri Msangi akizungumza na wananchi shuleni hapo.
============================================================
Habari/picha na Edwin Moshi, Makete.
Kufuatia
kukamilika kwa kiasi kikubwa majengo ya shule mpya ya sekondari ya
wasichana Makete iliyojengwa katika kijiji cha Utweve kata ya Ukwama
wilayani Makete, mkuu wa mkoa wa Njombe Kapteni mstaafu Asseri Msangi
ameagiza shule hiyo iandikishwe ili ianze kutumika.
Mkuu
wa mkoa ametoa agizo hilo hii leo Februari 11, 2014 wakati wa ziara ya
kukagua miradi mbalimbali ya elimu wilayani Makete, ambapo baada ya
kufika shuleni hapo ameridhishwa na ujenzi wa shule hiyo na kuona haina
sababu ya shule hiyo kuendelea kukaa bila kuandikishwa ili ianze kupokea
wanafunzi.
Akizungumza
na wananchi wa vijiji viwili vinavyojenga shule hiyo ambavyo ni Utweve
na Masisiwe, mkuu huyo wa mkoa mbali ya kupokea na kutjibu kero za
wananchi, amekasirishwa na tabia ya wazazi wa vijiji hivyo kuwaambia
watoto wao wafeli kwa makusudi ili wasiendelee na masomo ya sekondari.
"Ndugu
zangu dunia tuliyopo sasahivi, si ile tuliyoishi zamani, mtoto
asiposoma ni matatizo kwake, na ninyi wazazi wenye tabia ya kuwaambia
watoto wenu wafeli kwa makusudi mnatupelekea taifa letu kaburini na sisi
hatutakubali, tunaomba muiache hiyo tabia, somesheni watoto wenu"
alisema Msangi.
Katika
hatua nyingine Kapteni Msangi amechangia kiasi cha shilingi milioni 1
kwa ajili ya shule hiyo maalum kwa ajili ya wasichana kama njia mojawapo
ya kusaidia ujenzi wa shule hiyo ambayo inatarajiwa kuanza hivi
karibuni.
Shule
hiyo pekee ya wasichana wilayani Makete inajengwa na serikali kwa
kushirikiana na wazawa wa Makete wanaoishi nje ya wilaya hiyo, wananchi
pamoja na wadau mbalimbali.
No comments:
Post a Comment