MC Chaku (kushoto) akiwa na mmoja ya wakazi wa Mbagala tayari kwa kuchagua mshindi wa Championi Shinda Mahela.
…Kuponi za Championi Shinda Mahela zikiwa tayari kwa ajili ya droo.
Msimamizi wa Bodi ya Bahati Nasibu, Mrisho Milao (kushoto), Meneja Mkuu wa Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho (katikati) na kulia ni Ofisa Masoko wa Shinyanga Emporium, Herman Bernard wakiendelea kufuatilia droo.
..Mchezesha droo akichambua kuponi katika Viwanja vya Mbagaka Zakhem jijini Dar.
MC Chaku akimfunga kitambaa mkazi wa Mbagala ili amchague mshindi wa Championi Shinda Mahela
Msimamizi wa Bodi ya Bahati Nasibu, Mrisho Milao (kushoto) akikabidhiwa kuponi ya mshindi wa milioni 10 za Championi Shinda Mahela.
MC Chaku (kulia) na mkazi wa Mbagala wakitaja jina la mshindi wa milioni 10 za shindano la Championi Shinda Mahela ambaye ni Kizito George.
MC Chaku akimwaga kuponi za Championi Shinda Mahela wakati wa mchakato wa kumpata mshindi wa milioni 10.
…MC Chaku akiweka sawa kuponi hizo.
Msomaji wa Championi kutoka Mbagala akitafuta mshindi wa tisheti.
Mr Championi (kushoto) akimkabidhi mshindi tisheti.
…Wakazi wa Mbagala wakiendelea kufuatilia Bahati Nasibu ya shindano la Championi Shinda Mahela.
Wasomaji wakijaza kuponi za Championi Shinda Mahela kabla ya Bahati Nasibu kuanza.
Meneja Mkuu wa Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho (kulia) akiongea na wanahabari baada ya kupatikana mshindi wa Championi Shinda Mahela ambaye ni Kizito George.
Burudani wakati wa droo hiyo ya mwisho.
Burudani ikiwa imepamba moto Viwanja vya Mbagala Zakhem kabla ya droo ya mwisho ya kumpata mshindi wa milioni 10 kupatikana.
BAADA ya kusubiri kwa muda mrefu hatimaye, mshindi wa milioni 10 amepatikana kupitia droo ya Shinda Mahela na Championi ambaye ni Kizito George Chuka.
Droo hiyo iliyochezeshwa mbele ya Msimamizi wa Bodi ya Bahati Nasibu, Mrisho Milao kwenye Viwanja vya Mbagala- Zakhem jana Jumanne.
Akizungumza Kizito ambaye ni makazi wa Kawe jijini Dar alipopigiwa simu na muendeshaji wa shughuli hiyo MC Chaku, mshindi huyo alikuwa ndani ya daladala hivyo hakuwa na mengi ya kuongeza zaidi ya kushukuru kwa kujinyakulia kitita hicho.
Kizito, 43 alionekana kufurahia kutokana na sauti yake kusikika akichekelea na haijafahamika kama aliwasilimulia abiria wenzake aliokuwa nao ndani ya daladala hiyo.
Hata hivyo keshokutwa Alhamisi anatakiwa kuja Ofisi za Global Publishers kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kuchukua mkwanja wake huo.
“Nimefurahi sana lakini sasa hivi nipo ndani ya daladala naomba muda nikifika nitakupigia,” alisema Kizito.
Washindi wengine ambao walipatikana siku hiyo ni Athuman Yusuph, 40, mkazi wa Mwanza aliyejinyakulia shuka za kisasa na Amiri Kinguaba, 60 aliondoka na simu kali aina ya Samsung Galaxy.
(PICHA/HABARI: DENIS MTIMA NA LUCY MGINA/GPL)
======================================================
Mteja wa Benki ya NBC Kigoma aibuka mshindi wa droo kubwa ya promosheni ya Weka Upewe.
======================================================================Meneja katika Kitengo cha Kitengo cha Bidhaa za Kuwekeza na Wateja Wakubwa, Dorothea Mabonye akibonyeza kitufe ili kumpata mshindi wa droo kubwa ya promosheni ya Weka Upewe ya benki hiyo jijini Dar es Salaam leo. Mteja wa benki hiyo, Mary Malifedha Popote kutoka Kigoma amejishindia gari jipya aina ya Suzuki Swift lenye thamani ya shs milioni 28. Wengine kutoka kushoto ni Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GBT), Abdallah Hemedy, Meneja wa NBC Kanda ya Ziwa, Gaudence Shawa na Mkuu wa Huduma Rejareja za Kibenki wa NBC, Musa Jallow.
Mkuu wa Huduma Rejareja za Kibenki wa NBC, Musa Jallow (katikati) akizungumza katika hafla ya droo kubwa ya promosheni ya Weka Upewe ya NBC jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni, Meneja wa NBC Kanda ya Ziwa, Gaudence Shawa, Kaimu Mkuu wa Mtandao wa Matawi wa NBC, Raymond Mutagahywa na Meneja wa Kanda w NBC, Rachel Mwalukasa.
Meneja wa Kanda wa Benki ya NBC, Rachel Mwalukasa (katikati) akizungumza na mshindi wa droo kubwa ya promosheni ya Weka Upewe ya benki hiyo jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mtandao wa Matawi wa NBC, Raymond Mutagahywa na Mkuu wa Kitengo cha Kuwekeza na Wateja Wakubwa, Andrew Massawe.
============================================================
WAKAZI WA KATA YA MBUGANI WALILIA UMEME
Mahmoud Ahmad
Wakazi
wa kata ya mbugani mtaa wa mabatini kaskazini eneo la mwembe giza
wamekiomba chama cha mapinduzi katika kata hiyo na wafadhili
mbalimbali hapa nchini kuwasaidia mchango wa hali na mali katika
kufanikisha upatikanaji wa huduma ya umeme kwenye eneo lao kwa
kuwasaidia mchango wa kupata nguzo tano kati ya saba zinazohitajika.
Wakiongea
kwenye kikao chao cha ukusanyaji wa michango ya kupata huduma hiyo ya
umeme mbele ya katibu wa ccm wa kata hiyo Gerald Mashala wakazi hao
wamemuelezea kuwa wamejitahidi kukusanya fedha za kununulia nguzo mbili
hadi sasa lakini kutokana kipato chao kuwa kidogo wanakiomba chama cha
mapinduzi kuwasaidia upatikanaji wa nguzo tano iliwaweze kusogeza huduma
hiyo.
Pia
wakawataka wafadhili mbalimbali kusaidia upatikanaji wa hizo nguzo
tano za umeme ilikuweza kupata urahisi wa ufikaji wa eneo hilo kwani kwa
kipindi hichi wazee,wagonjwa na walemavu wamekuwa wakipata tabu
kutokana na giza na ufikaji wa eneo lao kwani lipo milimani.
“Unajua
ndugu mwandishi eneo letu lipo milimani na tunaishi na wazee,walemavu
na saa zingine wagonjwa na wajawazito kwa hali hii ni hatari kubwa sana
nyakati za usiku ufikaji wakeunakuwa wa shida hivyo kupitia wewe
tunaomba kupatwa huduma hiyo kwa haraka”alisisitiza Peter.
Hata hivyo CCM
kata hiyo imeahidi kutoa kiasi cha sh.200,000 katika jitihada za
kufanikisha juhudi za kujiletea maendeleo kwani wameonyesha juhudi kubwa
na hiyo ni kusaidia ilani ya chama hicho kufikisha asilimia
30%wawewamefikishiwa huduma ya umeme kwwa nchi nzima.
Mashalla
pia akasema atasaidia kwenda wafadhili mbalimbali wenye moyo wa
kusaidia maendeleo ilikuwezesha upatikanaji wa huduma hiyo huku
akiyaomba makampuni mbalimbali kusaidia kwa karibu jamii za pembezoni
ilikuweza kujiona hawajatengwa na jamii.
“Unajua
wakazi hawa ni sehemu ya wakazi wa kata hii wanaohitaji huduma
mbalimbali za kijamii ikiwemo huduma hii ya umeme na maji kwani
limekkuwa ni tatizo sugu huku mamlaka husika zikishindwa kukaa na jamii
kujua zitasaidiaje na hili ni tatizo”alisema mashalla.
===========================================================
NAIBU WAZIRI MAKALLA AENDELEE NA ZIARA MKOANI MOROGORO
=====================================
Naibu
Waziri wa Maji, Amos Makalla akisikiliza ripoti ya maji ya Wilaya ya
Morogoro katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, kushoto ni Mbunge
wa Morogoro Kusini, Innocent Kalogeris.
Mbunge wa Morogoro Kusini-Mashariki, Lucy Nkya akizungumza katika mkutano wa Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla wilayani Morogoro.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said Amanzi akizungumza katika mkutano wa Naibu Waziri wa Maji katika ziara yake wilayani hapo
Mbunge wa Morogoro Kusini, Innocent Kalogeris akizungumza na wakazi wa kijiji cha Bwira Chini katika ziara ya Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla katika jimbo lake, wilayani Morogoro.
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akizungumza na wananchi wa Bwira Chini katika ziara yake kijijini hapo, kushoto ni Mbunge wa Morogoro Kusini, Innocent Kalogeris na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said Amanzi.
Wakazi wa kijiji cha Bwira Chini wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla (hayupo pichani), wakati wa alipotembelea kijiji hicho katika ziara yake wilayani hapo.
………………………………………………………………………………………………….
Mbunge wa Morogoro Kusini-Mashariki, Lucy Nkya akizungumza katika mkutano wa Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla wilayani Morogoro.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said Amanzi akizungumza katika mkutano wa Naibu Waziri wa Maji katika ziara yake wilayani hapo
Mbunge wa Morogoro Kusini, Innocent Kalogeris akizungumza na wakazi wa kijiji cha Bwira Chini katika ziara ya Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla katika jimbo lake, wilayani Morogoro.
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akizungumza na wananchi wa Bwira Chini katika ziara yake kijijini hapo, kushoto ni Mbunge wa Morogoro Kusini, Innocent Kalogeris na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said Amanzi.
Wakazi wa kijiji cha Bwira Chini wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla (hayupo pichani), wakati wa alipotembelea kijiji hicho katika ziara yake wilayani hapo.
………………………………………………………………………………………………….
Naibu
Waziri wa Maji, Amos Makalla ameanza ziara yake mkoani Morogoro
Jumatano kwa kutembelea Mamlaka ya Mazingira na Majisafi Morogoro
(MORUWASA).
Mhe.
Makalla alifika MORUWASA na kujionea utendaji na kupata taarifa ya
mamlaka hiyo ambayo inatoa huduma ya maji mjini Morogoro na kukagua
miradi inayotekelezwa mkoa huo.
“Ninawaagiza
wakandarasi wahakikishe wanarudi kwenye maeneo yao ya kazi mara moja,
kama Waziri Maghembe alivyoagiza. La sivyo Serikali itaangalia taratibu
na kuchukua hatua kali. Na mkandarasi atayekaidi hatapata kazi sio tu
Wizara ya Maji, bali Tanzania nzima”, alionya Naibu Waziri.
“Muwe
karibu na kuwahudumia vizuri wateja na kuwe na ratiba nzuri ya mgao na
ya kueleweka na kwenye dharura mfike mara moja bila kuchelewa. Muondoe
urasimu usio wa lazima katika kutoa huduma kwa wananchi wote”, alisema
Makalla.
Pia,
alisema wananchi waiunge mkono Serikali katika kutunza mazingira na
vyanzo vya maji na amekuja Wizara ya Maji kutimiza sera za maji na
mipango ya Serikali katika sekta hiyo na si vinginevyo. Na kuahidi
kuwasilisha maombi yote aliyoyapokea Wizarani na kuyapapa msukumo
yafanyiwe kazi, isipokuwa yale yaliyo ndani ya uwezo wao wafanye bidii
kuyatatua.
Naibu
Waziri Alhamisi aliendelea na ziara hiyo katika Halmashauri ya Wilaya
ya Mvomero na kukagua baadhi ya miradi ikiwemo Kibati, Kwadoli na
Kagugu. Vilevile, ametembelea bwawa la Mindu na kijijiji cha Lusungu.
No comments:
Post a Comment