Nwa BFT Antony Mwangonda akiwa na makamu wa Rais Lukelo Willilo
………………………………………………………….. Na Mwandishi Wetu
MASHINDANO ya mchezo wa Ngumi yanayokwenda kwa jina la Nelson Mandela Open Championship yameanza kutimua vumbi katika
Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es salaam
akizungumzia mashindano hayo yalivyo na ubora wa hali ya juu Makamu wa Rais wa Shirikisho la ngumi za Ridhaa nchini ‘BFT’ Lukelo Willilo ‘amesema mashindano hayo kwa sasa yameboreshwa kwa kufuata taratibu za chama cha ngumi za ridhaa Dunia
kwa sasa mabondia hawavai kofia ngumu wanakuwa vichwa wazi hivyo
wapenzi wa ngumi weje waone mabadiliko makubwa katika ngumi za ridhaa
ndio ambazo ni msingi wa maendeleo ya mchezo wa masumbwi nchini;’
Zamani mabondia walikuwa
wanavaa kofia lakini kutokana na mabadiliko sasa hawavai kofia
wanapigana vichwa wazi ambapo kwa kuanzia tumeamua kuweka mashindano
haya kwenye viwanja vya wazi na ni bure tu hakuna kingilio ili kila mtu
ajionee mabadiliko ya ngumi mashindano hayo ambayo yanahusisha mikoa
mbalimbali nchini
Mashindano haya yatakuwa ya
siku tano kuanzia jumatano mpaka jumapili na ngumi zinaanza kupigwa saa
kumi na moja mpaka saa mbili usiku michezo ndiyo itakuwa ikiisha
Katika ufunguzi huo bondia
Patrck Kimweri wa Tanga alishindwa kufurukuta mbele ya Said Jabir wa
ngome na Rashidi Samvu wa Kigoma alipigwa kwa pointi na Hafidhi Kassimu
wakati Fabian Gaudence
akimsambalatisha Hussein Mnimbo |
No comments:
Post a Comment