Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko Rashid Salum Ali wa
kwanza (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar
PBZ wa kwanza (kulia) wakitia saini makubaliano ya ubadilishanaji
majengo ya Taasisi hizo mbili katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya
Benki ya Kiislamu ya PBZ Mpirani mjni Zanzibar. Katikati ni Mwenyekiti
wa Bodi ya PBZ Abrahamani Mwinyi.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko Rashid Salum Ali wa
kwanza (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar
PBZ wa kwanza (kulia) wakibadilishana hati ya makubaliano ya
ubadilishanaji majengo ya Taasisi hizo mbili ambapo PBZ itachukua jingo
la Ofisi ya Biashara ya Magari liliopo Malindi na Wizara ya Biashara
itachukua Jengo la Makao Makuu ya sasa ya PBZ la Darajani
Baadhi ya Maofisa wa PBZ wakiangalia utiaji saini wa makubaliano ya
ubadilishanaji wa majengo ya Benki hiyo na iliyokuwa Ofisi ya Shirika la
Biashara ya Magari lililochini ya Wizara ya Biashara, Viwanda na
Masoko.
Picha
ya pamoja ya maafisa wa PBZ na Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko
baada ya kumalizika hafla ya makubaliano ya ubadilishanaji wa majengo ya
Taasisi hzo mbili iliyofanyika Makao Makuu ya Benki ya kiislamu ya PBZ
Mpirani mjini Zanzibar.
Jengo
la Ofisi ya Biashara ya Magari liliopo Malindi Mjini Zanzibar ambalo
limekabidhiwa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kwa ajili ya kujenga Makao
Makuu Mapya ya Benki hiyo.
Jengo
la Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) liliopo Darajani Mjini Zanzibar
ambalo limekabidhiwa Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko.
(Picha na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar).
No comments:
Post a Comment