Afisa
mtendaji wa Kampuni ya DMB ambao ni wamiliki wa Maisha Plus Masoud Ally
(Masoud kipanya) Akitoa ufafanuzi namna ya mchujo unavyo fanyika ili
kuwapata vijana na akina mama watakao ingia katika Maisha Plus/Mama
shujaa wa Chakula, Wakati wa kufanya zoezi la kuwachagua wale
watakaoingia katika kijiji cha Maisha Plus 2013/2014.
…………………………………………………………………………………….
Fomu zaidi ya 4,000 za Mama Shujaa Maisha Plus zakusanywa
Majaji 9 kusimamia zoezi la kuchaguwa wakulima wanawake 20 na vijana 45
Majaji 9 kusimamia zoezi la kuchaguwa wakulima wanawake 20 na vijana 45
Zoezi la kuchaguwa washiriki wa
shindano la Mama Shujaa wa Chakula na Maisha Plus limeanza leo ambapo
zaidi ya fomu 4,000 zimekusanywa kutoka kwa washiriki.
Eluka Kibona, Meneja Utetezi na
Ushawishi wa Oxfam akiongea wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo alisema
zoezi la kupitia fomu litachukuwa siku nne kuanzia Jumatatu tarehe 3
hadi Alhamisi tarehe 6 Februari 2014. “Majaji walioteuliwa wana kazi
kubwa ya kupitia zaidi ya fomu 4,000 ambazo tumekishwazipokea na
nyingine bado zinawasili kutoka sehemu mbalimbali za nchi yetu. Baada ya
uchambuzi majaji watachaguwa wakulima wanawake 20 pamoja na vijana 45
ambao watashiriki kwenye shindano la mwaka huu. Majaji watasaidia
kuchambuwa fomu na vijana 17 waliojitolea kutoka Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam kitengo cha Jinsia. “
Jopo la majaji linajumuisha
waliobobea kwenye masuala yanayohusu kilimo, ufugaji, usalama wa
chakula, sera na utetezi, uchumi, biashara, vyombo vya habari, vijana na
maendeleo ya jamii.
Majaji ni kama wafuatavyo:
Rose Tesha Meneja Programu ya Maisha Salama shirika la VSO; Masoud Kipanya mwanzilishi wa shindano la Maisha Plus; Tatu Abdi Juma mshindi wa tatu shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2012 ; Francis Bonda Mkurugenzi wa kampuni ya DMB na mwanzilishi wa shindano la Maisha Plus, Edmund Matotay Mtafiti kutoka shirika la Oxfam; Anna Oloshoro mshiriki wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula mwaka 2011; Carolyn Kandusi mtaalamu wa jinsia kutoka shirika la PINGOS akitokea Loliondo; Zephaniah Mugittu mshauri wa mnyororo wa thamani wa mboga mboga anafanya kazi na shirika la Oxfam akitokea Lushoto, Tanga pamoja na Bernick Kimiro mshindi wa Maisha Plus 2012.

Washiriki wa Maisha Plus msimu
huu ni vijana wa miaka 21-26 kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Uganda,
Burundi na Rwanda wanaogombania kitita cha Fedha za kitanzania Milioni
25.
No comments:
Post a Comment