Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala, akifungua maji ya mradi wa kisima cha maji, Chang’ombe Unubini, wilaya ya Temeke.
Naibu
Waziri wa Maji, Amos Makala akizungumza na wakazi wa eneo la mradi wa
kisima cha maji cha Kichapwi, kata ya Kilakala, wilaya ya Temeke, kulia
ni Mwenyekiti wa mtaa wa Barabara ya Mwinyi, Yahya Mnali.
Wakazi
wa eneo la mradi wa kisima cha maji Kichapwi, kata ya Kilakala, wilaya
ya Temeke, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala (hayupo
pichani). Mradi wa kisima cha maji Tabata Segerea.
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala, akifungua maji ya mradi wa kisima cha maji, Chang’ombe Unubini, wilaya ya Temeke.
……………………………………………………………………………….
Naibu
Waziri wa Maji, Amos Makala, leo ameendelea na ziara yake ya jijini Dar
es Salaam kwa kukagua miradi ya visima vya maji inayosimamiwa na DAWASA
maeneo ya Temeke na Segerea.
Mhe.
Makala aliweza kufika kwenye miradi ya visima vya maji maeneo ya
Chang’ombe Unubini, Kichapwi na Segerea na kuona namna miradi hii
ilivyosaidia kutatua kwa kiasi kikubwa cha tatizo la maji katika maeneo
hayo ya jiji.
Naibu
Waziri aliridhika namna miradi hiyo ya kijamii, ambapo Serikali
ikishirikiana na wananchi wameweza kutekeleza mpango wa Serikali
kuhakikikisha inaleta ahueni kwa kutoa huduma za kuridhisha za maji
kufikia mwaka 2015.
“Napenda
kuwashukuru wananchi na DAWASA kwa kazi nzuri iliyofanyika katika
miradi hii, na ni dhahiri kuwa mpango wa kutoa huduma nzuri ya maji
jijini Dar es Salaam na nchi nzima inaendelea vizuri. Ningependa kuwaasa
wananchi wazidi kushirikiana kwa ukaribu na Serikali ili kuhakikisha
miradi hii inatunzwa na kuendelea kupanuka zaidi kwa ajili ya maendeleo
ya wananchi wenyewe na nchi nzima kwa ujumla”.
Vile
vile Mhe. Makala aliipongeza Kamati ya Jumuiya ya Watumia Maji ya Mradi
wa Kichapwi, Kilakala, wilaya ya Temeke kwa uendeshaji mzuri wa mradi
huo na kuweza kukusanya pesa nyingi, kiasi cha sh. Mil 11. Huku
wakifanikiwa kufungua akaunti mbili za benki kwa ajili ya makusanyo ya
mapato na rasilimali kama walivyoagizwa na DAWASA.
“Pamoja
na uchanga wake, Kamati ya Maji ya Kichapwi imefanya vizuri sana katika
kutekeleza majukumu yake na hakika ni mfano wa kuigwa nchini na kwa
kweli wanastahili pongezi nyingi”, alisema Naibu Waziri.
Mhe.
Makala atamaliza ziara yake ya siku tano jijini Dar es Salaam kesho,
kwa kutembelea maeneo ya Ubungo, na baada hapo kwenda Morogoro kuanza
ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi mkoani humo.
No comments:
Post a Comment