Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
akipokea maelezo ya hatua mbalimbali zilizofikiwa katika Ukarabati wa
Jengo la Ofisi za Utawala za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
toka kwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi
wa Magereza, Kibwana Kamtande (wa kwanza kushoto) alipotembelea hivi
karibuni Mjini Dodoma(wa kwanza kulia) ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Anne Makinda(wa pili kulia) ni Waziri wa Sera
na Uratibu wa Bunge. Mhe. William Lukuvi.
Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Anne
Makinda(katikati) akiwa ameongozana na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma,
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Kibwana Kamtande kabla ya
kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete alipotembelea kufanya ukaguzi wa Ukarabati wa Jengo la
Ofisi za Utawala za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo Mhe.
Rais ameonyesha kuridhishwa na kasi ya ukarabati unaofanywa na Jeshi l
Magereza kupitia Shirika lake la Magereza.
Mkuu
wa Magereza Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza
Kibwana Kamtande(wa kwanza kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na
baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza ambao wanasimamia kwa
karibu Ukarabati wa Jengo la Ofisi za Utawala za Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania linalokarabatiwa na Jeshi la Magereza kupitia
Shirika lake la Magereza ambapo hivi karibuni Mhe. Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameridhishwa na
kasi ya ukarabati wa Jengo hilo alipotembelea Mjini Dodoma(Picha zote na
Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
Hatua
mbalimbali iliyofikiwa ya ukarabati wa Jengo la Ofisi za Utawala za
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lililopo Mjini Dodoma ambapo
hivi karibuni Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete alifanya ukaguzi wa Ukarabati wa Jengo hilo na
kurudhishwa na kasi ya Ukarabati huo unaofanywa na Jeshi la Magereza
kupitia Kikosi chake cha Ujenzi kilicho chini ya Shirika la Magereza.
No comments:
Post a Comment