WIZARA YA MALIASILI NA UTALII KUSHIRIKI MAONESHO YA 40 YA BIASHARA YA KIMATAIFA SABASABA.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
Wizara
ya Maliasili na Utalii itashiriki katikaMaonesho ya40 ya Biashara ya
Kimataifa ya Dar es Salaam(SABASABA)kuanzia tarehe 28 Juni hadi tarehe 8
Julai, 2016 katika viwanja vya Mwalimu Julius.K.Nyerere, Dar es Salaam.
Wizara
itakuwa na washiriki kumi na sita (16) ambao ni Idara pamoja na Taasisi
zake mbalimbali. Idara zitakazoshiriki ni Utalii, Wanyamapori, Mambo ya
Kale na Misitu na Nyuki.
Kwa upande wa Taasisi ni Bodi ya
Utalii Tanzania (TTB), Chuo cha Taifa cha Utalii, Makumbusho ya Taifa,
Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya
Ngorongoro,Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI) na Vyuo vya
Wanyamapori (Mweka, Pasiansi na Likuyu Semaganga).
Taasisi
nyingine ni Vyuo vya Misitu na Nyuki (Olmotonyi, FITI Moshi na Chuo cha
Nyuki Tabora), Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Wakala wa Mbegu za
Miti, Taasisi ya Utafiti wa Misitu na Wadau wa Wizara ya Maliasili na
Utalii.
Washiriki wote hao watakuwa kwenye banda moja la
MALIASILI, Wizara inawakaribisha wananchi wote kwenye banda hilowaweze
kujionea na kuelimika namambombalimbali yanayohusu Utalii, Ufugaji wa
Nyuki, Uhifadhi wa Misitu, Malikale na Wanyamapori.
Aidha,
Wizara itatoa punguzo kwa watanzania kutembelea Hifadhi ya Taifa ya
Mikumikwa gharama nafuu. Safari ya kwenda na kurudi kwa watoto itakua
Tsh. 10,000 na watu wazima Tsh. 20,000. Safari ya kulala itakuwa Tsh.
50,000.
Pia katika maonesho hayo itakuwepo fursa ya kuwaona
wanyamapori hai mbalimbali kama vile Chui, Nyoka, Ndege wa aina
mbalimbali pamoja na SIMBA.
Kaulimbiu ya Maonesho hayo mwaka huu inasema“Tunaunganisha Uzalishaji wa Masoko”
No comments:
Post a Comment