CHAMA
cha mapinduzi, CCM, wilaya ya Arusha kimeziidi kujiimarisha mara baada
ya kukibomoa Chama cha Chadema, kufuatia hatua ya baadhi ya viongozi
waandamizi ngazi za kata kukihama na kujiunga na chama cha mapinduzi .
Viongozi hao wamejiunga na chama
cha mapinduzi kwa nyakati tofauti kwenye mikutano ya hadhara ya Chama
cha mapinduzi katika kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa
zinazoendelea nchini kote.
Miongoni mwa viongozi hao
walijiunga na Chama cha mapanduzi ni, aliyekuwa katibu wa Chadema, kata
ya sombetini, Abdi Madava,Gerad Majengo, aliyekuwa katibu kata ya
Terati, Prospa Mfinanga, aliyekuwa katibu, mwenezi kata ya Olerien
,Thomas willson aliyekuwa katibu kata ya Kaloleni, Emanuel Daniel,
aliyekuwa mwenyekiti wa Bavicha kata ya Kaloleni na Mussa
Lungo,aliyekuwa kamanda wa kanda ya kaskazini wa Chadema.
Uamuzi huo wa wanachama hao kukimbia Chadema kunazidi kukiweka pabaya chama hicho pamoja na UKawa na hivyo kukididimiza kabisa.
Akiwapokea wanachama hao wapya
katibu wa CCM, wilaya ya Arusha, Feruzy Bano, kwenye mikutano ya
hadhara, kwa nyakati tofauti,amesema viongozi hao wamefanya maamuzi
magumu ya kukubali kupoteza nyadhifa zao na kujiunga na chama cha
mapinduzi kutokana na ubora wa sera zake.
Kuanzishwa kwa vyama vingi ilikuwa ni fursa kwa kila ch
ama kutekeleza ahadi zao kwa
kuwatumikia wananchi lakini cha ajabu mpaka leo hakuna ahadi hata moja
iliyotekelezwa na vyama hivyo na badala yake vyama hivyo vimebakia
kuendesha siasa za maji taka ambazo ni za chuki zinazolenga
kuwachonganisha wananchi ili waichukie serikali yao.
Feruzi,amesema vyama hivyo
vilikuwa na fursa ya kuleta changamoto ya maendeleo nchini lakini
kutokana na kutokuwa na sera wala ilani za kuwatumikia wananchi
vimekuwa vitumikia matakwa ya watu na hivyo vimekuwa ni vyama vya watu
binafsi na sio vya kisiasa hivyo wanachama hawana sauti .
Akihutubia mikutanio wa hadhara
kwenye kata ya Sokon one wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo katibu wa
ccm, wilaya ya Arusha, Feruzy Bano, amesema Chama cha mapinduzi,
kinaendelea kutekeleza ahadi mbalimbali za kuwaletea wananchi maendeleo
hivyo akawaomba wananchi kuwachagua wagombea wa CCM.
Amesema Chama cha mapinduzi
kinatoa ahadi na kuzitekeleza tofauti na vyama vingine ambavyo tangia
vimeaanzishwa havijafanya lolote licha ya kupata ruzuku, na badala yake
vimebakia kulalama.
Kuanzishwa kwa vyama vingi
ilikuwa ni fursa kwa kila chama kutekeleza ahadi zao lakini cha ajabu
mpaka leo hakuna ahadi hata moja iliyotekelezwa na badala yake vyama
hivyo vimebakia kuendesha siasa za maji taka ambazo ni za maandamano.
Feruzi,ameongeza kuwa iwapo
nguvu kubwa ambayo inafanyika wakati wa maandamano ingelikuwa inatumika
katika maendeleo ni wazi kero nyingi zingelikuwa zimetatuliwa na
kutoweka kabisa.
Wakizungumza kwenye mikutano
hiyo kwa nyakati tofauti wanachama hao wapya wamesema walipotea njia
kujiunga Chadema, walienda kutokana na wimbi lililokuwepo na hivyo
walidhania kuwa wangelifikia malengo yao ya kisiasa wamegundua kuwa
wanapoteza muda hivyo wameamua kurejea CCM.
Walisema kuwa ndani ya Chadema
na UKawa kumejaa ubabauishaji na ubabe na kamwe vyama hivyo havina lengo
la kuwatumikia wananchi bali viongozi na wakawataka ambao hawajajiunga
na CCM kufanya hivyo haraka kwa kuwa CCM pekee ndicho chama chenye
misingi imara na uwezo wa kuondoa kero za wananchi.
No comments:
Post a Comment