Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Wataalam ya Afrika
katika masuala ya Majadiliano ya Mabadiliko ya Tabianchi kutoka nchini
Sudan, Nagmeldin El-Hassan, wakati alipokuwa akiwasili katika ukumbi wa
mikutano kwa ajili ya kuzungumza na wawakilishi wa Afrika katika mkutano
wa Mazingira Duniani (Cop20) unaoendelea jijini Lima, nchini Peru.
Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akizungumza na Wawakilishi wa Afrika katika mkutano wa Mazingira
wa Dunia (Cop20) (hawapo pichani) alipokuwa akiwahutubia leo Desemba
11, 2014. Katikati ni Waziri wa Mazingira wa Sudan, (kushoto) ni
Mwenyekiti wa Kamati ya Wataalam ya Afrika katika masuala ya Majadiliano
ya Mabadiliko ya Tabianchi kutoka nchini Sudan, Nagmeldin El-Hassan.
Picha na OMR Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza na Wawakilishi wa Afrika katika mkutano wa Mazingira wa
Dunia (Cop20) (hawapo pichani) alipokuwa akiwahutubia leo Desemba 11,
2014. katika mkutano wa Mazingira wa Dunia unaoendelea Jijini Lima,
nchini Peru.Katikati ni Waziri wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais,
Tanzania, Dkt. Binilith Mahenge. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akiagana na baadhi ya wawakilishi wa Afrika katika mkutano wa
Mazingira wa Dunia (Cop20) baada ya kuwahutubia leo Desemba 11, 2014,
katika Mkutano wa Mazingira Duniani na majadiliano kuhusu Mabadiliko ya
Tabianchi, unaoendelea jijini Lima, nchini Peru. Picha na OMR -Sehemu ya Wawakilishi wa nchi za Afrika katika mkutano wa Mazingira
Duniani, wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati
akiwahutubia leo, Desemba 11, 2014, mkutano wa Mazingira Duniani
(Cop20) unaoendelea jijini Lima, nchini Peru. Picha na OMR
Sehemu ya Wawakilishi wa nchi za Afrika katika mkutano wa Mazingira
Duniani, wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati
akiwahutubia leo, Desemba 11, 2014, mkutano wa Mazingira Duniani
(Cop20) unaoendelea jijini Lima, nchini Peru. Picha na OMR
-Sehemu ya Wawakilishi wa nchi za Afrika katika mkutano wa Mazingira
Duniani, wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati
akiwahutubia leo, Desemba 11, 2014, mkutano wa Mazingira Duniani
(Cop20) unaoendelea jijini Lima, nchini Peru. Picha na OMR
………………………………………………………………………………
Mheshimiwa Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal jana Desemba
10, 2014, amewahutubia wawakilishi wa Afrika katika Mkutano wa Mazingira
Duniani (Cop20) unaofanyika jijini Lima, nchini Peru. Mheshimiwa Makamu
wa Rais anahudhuria mkutano huu akimuwakilisha Rais Jakaya Kikwete
ambaye ni Kiongozi wa Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka Afrika kuhusu
Mabadiliko ya Tabia Nchi. Mkutano huo wa jana ulikuwa na dhima ya Afrika
baada ya mwaka 2015: Makubaliano Mapya kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi.
Awali Mheshimiwa Dkt. Bilal
aliwaambia wawakilishi wa Afrika katika mkutano uliojumuisha Mawaziri wa
Afrika wanaoshughulikia masuala ya Mazingira katika nchi zao kuwa,
Afrika licha ya unyonge wake bado inalo jukumu la kusimama kidete katika
kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na ili kufanikiwa katika jambo
hilo ni muhimu kwa Bara hili kuwa na sauti ya pamoja.
Mheshimiwa Makamu wa Rais
aliendelea kusema kuwa, Bara la Afrika lina kila sababu ya kuwa na
mipango yake ambayo itatumika kushirikisha nchi za nje ya Afrika ili kwa
pamoja Dunia iweze kuwa na kauli inayofanana yenye kulenga kukabiliana
na majanga yanayotokana na mabadiliko ya Tabia Nchi licha ya kuwepo
tofauti za kimaendeleo kati ya Afrika na nchi za mabara mengine.
Awali akizungumza kabla ya
Mheshimiwa Makamu wa Rais, Waziri wa Mazingira wa Sudan ambaye ni
Mwenyekiti wa kundi hili la Afrika Dkt. Hassan Albdelgadir Hillal
alisema, kundi la Afrika linapongeza uongozi wa Tanzania kupitia kwa
Rais Jakaya Kikwete kwa namna unavyosimamia agenda hizi za mabadiliko ya
Tabia Nchi na kusimamia upatikanaji wa sauti moja kutoka kwa nchi za
Afrika. Dkt. Abdelgadir aliendelea kusema kuwa, Afrika inatakiwa kutumia
mkutano huu wa Lima kwa umakini ili kuhakikisha mipango inayofikiwa
inapata kutambulika na kuonekana mwakani wakati mkutano kama huu
utakapofanyika jijini Paris.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Binilith Mahenge ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Mawaziri wa Mazingira kwa nchi za Afrika yeye alibainisha
kuwa, viongozi wa nchi za Afrika wamekuwa mstari wa mbele kabisa
kuhakikisha kuwa Afrika inasikika na kwamba anatarajia ushirikiano
katika ngazi ya Mawaziri kuendelea hata pale atakapokuwa anakabidhi
nafasi hiyo kwa Waziri wa Mazingira wa Misri.
Katika mkutano mwingine ambao
pia ulikuwa mwendelezo wa Siku ya Afrika katika COP20, Mheshimiwa Makamu
wa Rais Dkt. Bilal alisisitiza kuwa Afrika inatakiwa kuhakikisha vijana
na akina mama wanakuwa mstari wa mbele katika kukabiliana na hali hii
ya mabadiliko ya tabia nchi.
“Makundi haya ni muhimu sana kwa
kuwa ndiyo yanayohusika moja kwa moja na shughuli za kila siku.
Hatutaweza kufanikiwa kama tutayaacha makundi haya nyuma,” alisema
Mheshimiwa Makamu wa Rais katika Mkutano huo ambao pia ulihutubiwa na
Dkt. Fatima Denton, Mkurugenzi wa Harakati Maalum kutoka Shirika la
Umoja wa Mataifa la Kamishenbi ya Uchumi kwqa Afrika (UNECA).
No comments:
Post a Comment