Katibu wa chama cha mapinduzi mkoani iringa HASSANI MTENGA akiwahutubia wananchi wa mataa wa semtema mjini iringa
Na fredy mgunda, iringa
Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM
mkoani Iringa HASSANI MTENGA, amefungua rasmi kampeni za uchaguzi wa
Serikali za mitaa katika mtaa wa semtema mkoani iringa.
Akiwahutubia mamia ya wananchi wa mtaa wa semtema MTENGA
aliwataka wananchi wa eneo hilo kuwa makini wakati wa kuchagua kiongozi
katika uchaguzi utakao fanyika tarehe 14/12/2014.
MTENGA alisema kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa ni muhimu
sana kwa maendeleo ya nchi na watu binafsi kwa kuwa kila maendeleo
yanaanzi chini ndio yanaenda juu,hivyo wananchi wanatakiwa kuwa makini
sana na kumchagua kiongozi anayefaa.
aidha MTENGA aliwataka wanafunzi wa vyuo vikuu mkoani
iringa kuacha kuiga siasa chafu ambazo waiga kutoka kwa wapinzani wao
kwa kuwa wanaiga kitu ambacho hawakijua ambacho kitawaletea madhara
baadae.
alisema kuwa IRINGA ni ya watu wa iringa hivyo kuwaambia
wanafunzi wa vyuo vyote mkoani iringa kuwaachia siasa wana iringa na wao
waendelee na walicho kifuata hapa na sio isasa.
kwa upande wake wanafunzi waliohudhuria mkutano huo
walimsifu katibu huyo wa chama cha mapinduzi kwa kuwa na sera
zinazotekeleza na kuwaambia ukweli vijana waliopo vyuoni kwqa kuwa
wananfunzi wengi wamekuwa wakiiga mambo mengi bila kujua nini kipo mbele
yao.
lakini wananchi waliojitokeza
eneo hilo walimuita katibu huyo kwa jina dawa ya muarobaini kwa maneno
aliyoyatoa katika mkutano huo na kumsifu kiongozi huyo kuwa ni kiongozi
ayefaa kuigwa hapa mkoani iringa.
pia kunabaadhi ya wananchi
walisikika wakisema kwa sera za katibu MTENGA mbunge wa jimbo la iringa
mjini atake asitake ataondoka tu na kumwomba aanze kukusanya kilicho
chake.
No comments:
Post a Comment