Meneja
wa kituo cha Kahama FM Redio, Marco Mipawa (kushoto) akielekea kukwea
pipa kuelekea nchini Ghana kwenye ziara ya mafunzo ya wiki mbili.
Na Marco Mipawa, Accra- Ghana
Tanzania
inaweza kuwa nchi ya kwanza katika maendeleo ya uchumi iwapo itaweka
sera madhubuti za uzalishaji wa Gesi na kuwa na viongozi wenye dhamira
dhabiti ya kuiendeleza nchi na kuboresha maisha ya watu.
Haya
yamebainishwa na Meneja wa Redio Kahama FM Marco Mipawa leo wakati
akiendelea na ziara ya mafunzo nchini Ghana ya kujionea jinsi vyombo vya
habari vinavyofanya kazi na jamii katika suala zima la maendeleo.
Mipawa
ameyasema hayo baada ya kuona kuwa nchi ya Ghana inalo tatizo kubwa la
upatikanaji wa nishati ya umeme hata kuliko Tanzania inavyoathirika na
tatizo hilo lakini maisha ya watu ni mazuri na uchumi uko juu.
Amesema,
katika jiji la Accra umeme hukatika takriban robo tatu ya siku na
matumizi ya jenerata ni makubwa lakini thamani ya pesa yao iko kubwa
ikilinganishwa na ya Tanzania ambapo kukatikakatika kwa umeme ni mara
chache.
Mipawa
amesema, dola moja ya marekani inathamanishwa na Sedisi tatu za Ghana
ikiwa ni sawa na Shilingi 1770 za Tanzania hali inayoonyesha uchumi wa
Tanzania uko chini ukilinganishwa na wa Ghana.
Baadhi
ya wananchi wa Accra wamemwambia Mipawa kuwa, kinachoisaidia nchi ya
Ghana ni Uzalishaji mali katika kilimo, madini na ufugaji; huku sera na
sheria za nchi zikisimamiwa kwa umakini mkubwa kwa maslahi ya nchi.
Wamesema
suala la kudhibiti rushwa na kusimamia utii wa sheria vikiambatana na
uwazi na ukweli wa serikali na viongozi wa Ghana, ndiyo silaha mahususi
zilizoifanya Ghana kuwa na uchumi imara na maisha mazuri ya watu.
Ziara
ya mafunzo ya wiki mbili ya kujionea utendaji wa vyombo vya habari
nchini Ghana, imehusisha watu tisa kutoka Tanzania wakiwemo waandishi wa
habari na viongozi wa vyombo vya habari mbalimbali kwa udhamini wa
Tanzania Media Fund (TMF).
No comments:
Post a Comment