Na Kibada Kibada Katavi
Jeshi la Polisi Mkoani Katavi
limeonya kuwa halitasita kuwachukulia hatua kali za kisheria kwa mtu
yeyote au kikundi cha chochote cha watu watakaojihusisha na Vitendo vya
Vurugu, fujo ama Vitisho vinavyoweza kusababisha uvunjifu wa amani
wakati wa zoezi zima la uchaguzi wa viongozi wa Serikali za mitaa.
Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi
Kamishina Msaidizi wa Polisi Dhahiri Kidavashari katika Taarifa yake
kwa vyombo vya Habari ameeleza kuwa Jeshi limejipanga vizuri kwa
kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na Usalama kuhakikisha kwamba
hakuna vitendo vyovyote vya uvunjifu wa amani vitakavyojitokeza wakati
wa Kampeni na hata siku ya kupiga kura na pale ambapo vitajitokeza
vitadhibitiwa kwa haraka na wahusika kukamatwa na sheria kuchukua mkondo
wake.
Amesema ulinzi umeimarishwa
katika maeneo yote na wananchi wasiwe na hofu, katika kipindi hiki
chote cha kampeni za uchaguzi wa serikali za Mitaa na hasa siku ya
upigaji kura.
Kamanda Kidavashari akawashauri
wale wote waliojiandikisha kupiga kura wajitokeze siku ya kupiga kura
bila hofu ya aina yeyote. Na kusisitiza kuomba ushirikiano kwa jamii na
kutoa taarifa za mtu ama vikundi vya aina yeyote vinavyojihusisha na
vitendo vya vitisho ,vurugu na fujo dhidi ya wananchi waliojiandikisha
kupiga kura ili hatua kali za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao
mapema.
Katika hatua nyingine kampeni za
kuwanadi wagombea kwa vyama vyote mkoani katavi zimeendelea huku kukiwa
kunaripotiwa kuwepo kwa dallili za makundi Fulani kujipenyeza kutaka
kuvuruga uchaguzi siku ya kupiga kura hata hivyo atakayekamatwa
atashughulikiwa kwa mjibu wa sheria za nchi.
No comments:
Post a Comment