Katibu
Mkuu wa jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) na
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Ndugu Sixtus Mapunda anategemea
kufanya ziara ya siku na nne (14) katika mikoa minne ya Kanda ya Ziwa,
ambayo ni Tabora, Shinyanga, Geita na Kagera kuanzia kesho tarehe 12st Dec 2014.
Ziara
hii ya kikazi ya Katibu Mkuu inalenga kukagua na kuhimiza ujenzi na
uimara wa jumuia ya Vijana katika maeneo husika lakini pia kushiriki
kampeni zinazoendelea za uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa
kufanyika mnamo tarehe 14th Dec 2014.
Pia,
Katibu Mkuu anatarajia kufanya mikutano ya ndani na viongozi wa Jumuiya
na Chama, pia kufanya mikutano ya hadhara inayolenga kuingiza wanachama
wapya ndani ya jumuiya na chama kwa ujumla.
Kuhimiza
wanachama wa chama cha mapinduzi na viongozi kuwaandaa wananchi katika
kuipigia kura katiba mpya iliyopendekezwa wakati ukifika.
Ziara hiyo ya Katibu Mkuu inategemea kumalizika tarehe 25th Dec 2014
No comments:
Post a Comment