NA MWANDISHI WETU,TANGA.
TIMU ya soka Coastal Union ya
Tanga inatarajia kusheherekea miaka hamsini na nne ya Uhuru wa Tanzania
kwa kucheza mechi ya kirafiki na timu ya AFC ya Arusha itakayochezwa
kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani Desemba 9 mwaka huu.
Mechi hiyo ni maandalizi kwa timu
hiyo kujiandaa na mechi zake za Ligi kuu soka Tanzania bara baada ya
mapumziko ya siku kumi kutokana na Ligi kuu kusimama kwa muda ambapo
itaendelea Desemba 26 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari
leo,Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema kuwa mechi hiyo
itakuwa ni muhimu kwa timu hiyo kujitayarisha kwa ajili ya raundi
inayofuata kwenye michuano hiyo.
Amesema kuwa baada ya kumalizika
mechi hiyo wataangalia uwezekano wa kutafuta mechi nyengine ya majaribio
kabla ya kuanza ligi hiyo ambayo msimu huu imeonekana kuwa na upinzani
mkubwa
Aidha amesema kuwa timu hiyo ya
AFC yenye makazi yake Mkoani Arusha inatajiwa kuwasili mkoani Tanga
Desemba 8 mwaka huu kwa ajili ya mtanange huo lengo likuwa kuziandaa
timu zote mbili kwa mashindano yanayowakabili.
Amesema kuwa mechi hiyo ina
umuhimu kwa timu zote mbili sisi ni kujiandaa na Michuano ya Ligi kuu
Tanzania bara raundi inayofuata na wapinzania wetu wanajiandaa na Ligi
daraja la kwanza hapa nchini.
Hata hivyo amesema kuwa mazoezi ya
timu hiyo yameendelea kushika kasi kwenye viwanja vya Mkwakwani mjini
Tanga baada ya wachezaji wote waliokwenda mapumziko kurejea kwa asilimia
kubwa.
No comments:
Post a Comment