Na MatukiodaimaBlog
.WANANCHI wa kitongoji cha Dodoma kijiji cha Amani wilaya
ya Ludewa mkoani Njombe kuondokana na kero ya maji safi na salama
baada ya mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kuwatimizia ahadi
yake ya vifaa vyenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 14. 5 kwa ajili
ya kuvuta na kusambaza maji safi na salama ya bomba katika kitongoji
hicho .
Akishukuru kwa niaba
ya wananchi wengine wakati wa hafla ya kukabidhiwa vifaa hivyo
jana Bi Belinada Mwenda alisema kuwa awali wananchi wapatoa zaidi ya
600 wa kitongoji hicho ambacho kimeanzishwa na jamii ya wachimbaji
wa madini ya dhahabu ,walikuwa wakitumia maji machafu yanayotumika
kuoshea madini na kunyweshea mifuko .
Hivyo alisema kuwa
msaada huo wa maji safi na salama utasaidia kuwaepusha na magonjwa
na milipuko kama kuhara na mengine ambayo walikuwa wakiyapata
kutokana na matumizi ya maji yasiyo salama kwa afya ya binadamu kwa
kipindi chote cha zaidi ya miaka 10 sasa toka kitongoji hicho
kilipoanzishwa mwaka 1992.
” Hakika
tunakushukuru sana mbunge wetu kwa kutusaidia msaada wa vifaa hivi
kwa ajili ya maji …..toka mwaka 1992 hadi leo tumekuwa tukiteseka
kwa magonjwa mbali mbali na hata baadhi yetu kupoteza maisha
kutokana na matumizi ya maji machafu ambayo tulikuwa tukitumia maji
ambacho kimsingi yalikuwa ni mabaki ya maji yanayobaki katika
kunyweshea mifugo na kuoshea madini”
Bi Mwenda alisema
wananchi hao mbali ya kero kubwa ya maji ambayo walikuwa wakiipata
ila bado walionyesha uaminifu kwa mbunge wao kwa kuendelea kubaki
ndani ya CCM hadi sasa wanapotimiziwa ahadi yao hiyo kwa kitongoji
hicho kuwa ni moja kati ya vitongoji vyenye msimamo na mbunge wao kwa
kutoviunga mkono vyama vya upinzani .
” Kwa shida tuliyokuwa
tukiipata kama maeneo mengine leo wote tungekuwa tumejiunga na
upinzani ila tuliamini chama pekee ambacho kinaweza kutusaidia na CCM
na ndio sababu hatukuona sababu ya kujiunga na vyama vya upinzani
…..mheshimiwa mbunge wetu tunakuhakikishia kuwa kitongoji hiki hakuna
hata mwananchi mmoja ambae ni upinzani na wala hatuna mpango wa
kuhangaika na vyama sisi tutabanana hapa hapa CCM”
Akizungumza na
wananchi hao mbunge Bw Filikunjombe pamoja na kuwapongeza kwa
kutojiunga na vyama vya upinzani bado alisema kuwa ameguswa kutimiza
ahadi yake kwa wakati kutokana na mateso makubwa ambayo wananchi hao
walikuwa wakiyapata kwa kukosa huduma ya maji safi na salama .
Kwani alisema kuwa
lengo la serikali ya CCM iliyopo madakarani chini ya Rais Dr Jakaya
Kikwete ni kuona watanzania wanaendelea kuboreshewa mazingira ya
maisha yao na hata kupunguza baadhi ya kero zinazoweza kupunguzw kwa
wakati uliopo na ndio sababu ya yeye kama mbunge pia kuendelea
kukimbiza kasi ya maendeleo ya jimbo hilo la Ludewa na kamwe hatakubali
kuona wananchi wake wakiendelea kuteseka.
“Ndungu zangu
wananchi wa kitongoji hiki cha Dodoma katika kijiji hiki cha
Amani nimewapenda sana na ninyi wenyewe mnatambua kuwa mimi mbunge
wenu nawapenda ….. hivyo msaada huo leo ni utekelezaji wa ahadi yangu
niliyoitoka miezi michache iliyopita nikiwa kama mbunge wenu japo
siku nilipotoa ahadi hii baadhi yenu hamkuweza kuamini kama leo
ingetekelezwa …nawaombeni sasa tunzeni vema vifaa hivi na kutunza
zaidi mazingira ili kufanya chanzo cha maji kuendelea kuwa hai
zaidi “
Mbunge Filikunjombe
alivitaja vifaa ambavyo amevitoa ni pamoja na bomba za maji ambazo
zitasambazwa katika kitongoji chote kutoka kwenye chanzo cha maji
zaidi ya kilometa 20 hadi kwenye kitongoji hicho .
Kuhusu wafugaji
wanaochungia mifugo katika chanzo cha maji mbunge huyo aliwataka
wananchi na viongozi hao kuweka sheria ya kulinda chanzo hicho
cha maji vinginevyo hakutakuwa na maana ya kuwa na bomba za maji
safi ambazo zitaingiliwa na mifugo.
|
No comments:
Post a Comment