WAIMBAJI watakaoimba kwenye
Tamasha la Krismasi katika mikoa ya Mbeya, Iringa na Songea wanatarajia
kupigwa msasa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), kupitia semina
itakayofanyika Desemba 17 katika ofisi za Msama Promotions, Kinondoni
jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo, Abihud Mang’era semina hiyo itahusisha baadhi ya watendaji wa Basata ambao watafikisha ujumbe wa serikali katika tasnia ya muziki.
Mang’era alisema ni muhimu kwa waimbaji kuhudhuria semina hiyo ambayo ina lengo la kuwapa mwangaza waimbaji ambao watashiriki kutoa huduma ya neno la Mungu.
“Ni muhimu kwa waimbaji kuhudhuria katika semina hiyo ambayo itaongozwa na watendaji wa Basata ambao watashirikiana na watendaji wa Msama Promotions,” alisema Mang’era.
Mang’era alisema semina hiyo itawasaidia waimbaji kukumbuka masuala ya msingi pindi wawapo jukwaani ambako alisisitiza waimbaji kuhudhuria semina hiyo.

No comments:
Post a Comment