Katibu
Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bibi Mary Massay
akitambulisha meza kuu wakati wa maadhimisho ya Siku ya haki za binadamu
yaliyoenda sambamba na mkutano wa kujadili utekezaji wa makubaliano ya
haki za binadamu nchini na maandalizi ya ripoti ijayo yaliyofanyika jana
jijini Dar es Salaam.(Picha na Zainul Mzige wa MOblog).
Na Mwandishi wetu
MRATIBU
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
ameitaka serikali ya Tanzania pamoja na mafanikio makubwa katika
kufanikisha amani na kutia saini mikataba ya kimataifa ya haki za
binadamu, kufanyia kazi maeneo kadhaa ambayo bado yanatishia sifa nzuri
ya taifa hili.
Maeneo hayo ni mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi, wanawake vikongwe na ukatili kwa watoto.
Alisema taifa hili ambalo limekuwa kimbilio la wakimbizi,kuukubali kuwa
makao ya mahakama mbili kubwa za kimataifa zinazoshughulikia haki za
binadamu (ICTR na African Court of Human rights) sasa linashuhudia
madhila kwa baadhi ya wananchi wake ambao huuawa kwa imani za kijinga.
Akizungumza
katika siku ya mataifa ya haki za binadamu mjini hapa, Mratibu huyo
pamoja na kutoa ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, alisema ili
Tanzania iweze kutekeleza kwa umakini kauli mbiu ya mwaka huu “haki kwa
wote siku zote 365” maeneo yaliyotajwa yanastahili kufanyiwa kazi kwani
ni changamoto kubwa.
Mgeni
rasmi Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mh Ali
Hassan Rajab akizungumza wakati wa akifungua mkutano wa kujadili
utekezaji wa makubaliano ya haki za binadamu nchini na maandalizi ya
ripoti ijayo ulioenda sambamba na maadhimisho ya siku ya haki za
binadamu duniani.
Alisema
Tanzania ambayo imetia saini na kuridhia mikataba ya haki za binadamu
kama ya kuwatambua walemavu, kukabili ubaguzi dhidi ya wanawake (CEDAW)
na ule wa kulinda haki za watoto (CRC) inaposherehekea siku ya haki za
binadamu inakabiliwa na doa hilo la ukatili miongoni mwa watu wake.
Alisema
ipo haja ya kuimarisha usalama wa makundi hayo kwa kuhakikisha kwamba
mashauri yao mahakamani yanamalizika na haki kuonekana kutendeka .
Alisema
familia ambazo zimepoteza watu wake kwa namna ya kikatili wanahitaji si
tu kuona haki inatendekea bali wahusika wake wakichukuliwa hatua na
ulinzi kwa makundi hayo ukiimarishwa.
Aidha
alisema kwamba anapata maumivu makubwa anaposikia kuwapo na taarifa
nyingi za ukatili kwa watoto na kuendelezwa kwa mila mbaya zinazofunika
haki za msingi huku wahusika wakiwa hawachukuliwi hatua au upelelezi
ukidaiwa bado kukamilika.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisoma
hotuba kwenye maadhimisho ya siku ya haki za binadamu duniani yaliyoenda
sambamba na mkutano wa kujadili utekezaji wa makubaliano ya haki za
binadamu nchini na maandalizi ya ripoti ijayo.
Alisema
kitendo cha kuchelewesha haki kutokana na upelelezi kutokamilika au
kushindikana kutokana na kukosekana kwa fedha au familia zenyewe
kushindwa kutafuta haki kutokana na kutokuwa na fedha kunavuruga jina
zuri la nchi hii ambayo ina makabila mengi na tamaduni tofauti.
Alisema
pamoja na ukweli kuwa matendo hayo kisheria ni haramu kukosekana kwa
utashi kwa viongozi kukabiliana na changamoto zilizopo na kuachwa kwa
mila mbaya kunawafanya wananchi wabaki katika mazingira ya kutotendewa
haki.
Alisema mfumo wa sheria lazima uonekane kufanya kazi ili kukabiliana na wavunjaji wa haki za binadamu.
“Ni
matumaini yangu kwamba serikali ya Tanzania itaonesha kuwajibika kwake
na kuhakikisha inaangalia changamoto hizi na kuziondoa ili kuwezesha
kutekeleza haki za binadamu saa 24, siku saba za juma na siku 365 za
mwaka” alisema na kuahidi kwamba Umoja wa mataifa katika hilo utaendelea
kutoa ushirikiano.
Mkuu
wa Balozi za Umoja wa Ulaya (EU) nchini Tanzania na Afrika Mashariki,
Mh. Filiberto Ceriani-Sebregondi akizungumza kwenye maadhimisho ya siku
ya haki za binadamu duniani yaliyoenda sambamba na mkutano wa kujadili
utekezaji wa makubaliano ya haki za binadamu na maandalizi ripoti ijayo.
Aidha
alisema kwamba UN itaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania
kuimarisha kamisheni ya haki za binadamu na utawala bora (CHRAGG) na
taasisi nyingine za kijamii kuhakikisha kwamba kuna mfumo wa kulinda
haki za biandamu.
Aidha
mratibu huyo ameitaka serikali ya Tanzania kukamilisha uongozi wa
CHRAGG na pia kuangalia watetezi wa haki za binadamu wanapata ulinzi wa
kutosha dhidi ya watu wanaowatishia maisha.
Naye
Mkuu wa Balozi za Umoja ya Ulaya (EU) nchini Tanzania na Afrika
Mashariki Filiberto Ceriani-Sebregondi ameitaka serikali ya Tanzania
kuangalia mapendekezo matatu iliyokataa ambayo yanagusa haki za
binadamu.
Mapendekezo hayo yalikuwamo katika mfumo wa Umoja wa mataifa wa kupitia mambo mbalimbali yanayohusu haki za binadamu (UPR).
Meza
kuu kutoka kushoto ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na
Utawala Bora, Bibi Mary Massay, Mkuu wa Balozi za Umoja wa Ulaya (EU)
nchini Tanzania na Afrika Mashariki Filiberto Ceriani-Sebregondi, mgeni
rasmi Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mh Ali
Hassan Rajab na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na
mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini,
Alvaro Rodriguez katika maadhimisho ya siku ya haki za binadamu duniani
yaliyoenda sambamba na mkutano wa kujadili utekezaji wa makubaliano ya
haki za binadamu na maandalizi ripoti ijayo.
Balozi
huyo alitaja mapendekezo hayo ni pamoja na kufuta adhabu ya kifo,
kuweka umri unaoruhusu ndoa na kuchukua hatua za kulinda waandishi wa
habari na kulinda utamaduni wa wananchi wake.
Alisema mambo hayo ni sehemu muhimu ya kutekeleza maazimio ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu.
Aidha
balozi huyo pia aliitaka serikali kukamilisha kamisheni ya haki za
binadamu na utawala bora na kuiwezesha kufanyakazi zake zinazopaswa
ikishirikiana na asasi za kiraia na wadau wengine wa haki za binadamu.
Hata hivyo alisema jumuiya hiyo itaendelea kufanyakazi na serikali katika kuhakikisha kwamba haki za binadamu zinazlindwa.
Hata
hivyo balozi huyo amesema ni vyema kuendelea kuyafanyia kazi mapendekezo
mengine 119 ambayo serikali ilikuwa imeyakubali na kuonesha mafanikio
yake katika majadiliano yajayo.
Pichani
juu na chini ni baadhi ya mabalozi, wadau wa haki za binadamu na wageni
waalikwa wakifuatilia hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolewa katika
maadhimisho ya siku ya haki za binadamu duniani yaliyoenda sambamba na
mkutano wa kujadili utekezaji wa makubaliano ya haki za binadamu na
maandalizi ripoti ijayo.
Nkason
Sarakikya kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali akitoa tathmini
ya hali ya haki za binadamu Tanzania kwenye maadhimisho ya siku ya haki
za binadamu duniani yaliyoenda sambamba na mkutano wa kujadili utekezaji
wa makubaliano ya haki za binadamu na maandalizi ripoti ijayo.
Balozi
Mdogo anayeshughulikia masuala ya habari na siasa kutoka Jumuiya ya
Ulaya Tanzania, Bi. Laura REALE, akiuliza swali kuhusiana na uboreshaji
wa sheria ya ndoa za utotoni kwenye mkutano wa kujadili utekezaji wa
makubaliano ya haki za binadamu na maandalizi ripoti ijayo wakati
maadhimisho ya siku ya haki za binadamu duniani.
Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani
(UNFPA), Dkt. Natalia Kanem akizungumza kwenye mkutano huo wa kujadili
utekezaji wa makubaliano ya haki za binadamu na maandalizi ripoti ijayo.
Dr.
Khoti Kamanga kutoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Kitivo cha sheria
akitoa maoni kwenye mkutano wa kujadili utekezaji wa makubaliano ya haki
za binadamu na maandalizi ripoti ijayo.
Mtaalam
wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce
Temu (katikati), Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa
(UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama pamoja na Afisa Habari wa Umoja wa ulaya
Tanzania (EU), Susanne Mbise (kushoto) katika picha ya pamoja.
Mkuu
wa Balozi za Umoja wa Ulaya (EU) nchini Tanzania na Afrika Mashariki,
Mh. Filiberto Ceriani-Sebregondi (kushoto) akiteta jambo na Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
(katikati). Kulia ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na
Utawala Bora, Bibi Mary Massay.
Mratibu
wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu THRDC Taifa, Bw. Onesmo
Olengurumwa akiteta jambo na Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mh.
Lennarth Hjelmaker wakati wa mkutano wa kujadili utekezaji wa
makubaliano ya haki za binadamu na maandalizi ripoti ijayo ulioenda
sambamba na maadhimisho ya siku ya haki za binadamu duniani.
Balozi
wa Ujerumani nchini Tanzania, Mhe,Egon Kochanke ( wa pili kushoto)
akibadilishana mawazo na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mh. Diana
Melrose (wa pili kulia) pamoja na wakili wa serikali ya mapinduzi
Zanzibar, Bw. Othman Suleiman wakati wa maadhimisho hayo.
Katibu
Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bibi Mary Massay
(kushoto) akiongozana na Mkuu wa Balozi za Umoja wa Ulaya (EU) nchini
Tanzania na Afrika Mashariki, Mh. Filiberto Ceriani-Sebregondi
(katikati) pamoja na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na
mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini,
Alvaro Rodriguez kuelekea sehemu maalum kwa ajili ya picha ya pamoja na
washiriki wa mkutano wa kujadili utekezaji wa makubaliano ya haki za
binadamu na maandalizi ripoti ijayo katika kuadhimisha siku ya haki za
binadamu duniani.
Mgeni
rasmi Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mh Ali
Hassan Rajab (wa pili kulia waliokaa) katika picha ya pamoja na wadau
waliohudhuria mkutano wa kujadili utekezaji wa makubaliano ya haki za
binadamu na maandalizi ripoti ijayo ulioenda sambamba na maadhimisho ya
siku ya haki za binadamu duniani.
Balozi
wa Ireland Nchini Tanzania, Mh. Fionnuala Gilsenan (kulia)
akibadilishana mawazo na Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na
Utawala Bora, Bibi Mary Massay (kushoto) mara baada ya zoezi la picha ya
pamoja. Katikati ni Mshauri mwandamizi wa haki za binadamu kutoka Umoja
wa Mataifa Tanzania, Chitralekna Massey.
No comments:
Post a Comment