Meneja
Uhusiano wa Kampuni ya Airtel Tanzania,Jackson Mmbando akiongea na
waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi huduma mpya ya
HOME WI-FI itakayowawezesha wateja wake watumiaji INTANETI kufurahia
kutumia kifurushi kimoja familia nzima kwa kuwaunganisha na Wi-fi watu
32 ndani ya familia na kuunganisha wanafamilia wengine wanne waliopo
mahali popote nchini Tanzania kufurahia internet ya 3.75G. kulia ni
Meneja Masoko wa Airtel Home WiFi,Gaurav Dhingra.
Meneja
Masoko wa Kampuni ya Airtel Home WiFi,Gaurav Dhingra (katikati)
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi
huduma mpya ya HOME WI-FI itakayowawezesha wateja wake watumiaji
INTANETI kufurahia kutumia kifurushi kimoja familia nzima kwa
kuwaunganisha na Wi-fi watu 32 ndani ya familia na kuunganisha
wanafamilia wengine wanne waliopo mahali popote nchini Tanzania
kufurahia internet ya 3.75G. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Kampuni ya
Airtel Tanzania,Jackson Mmbando na kushoto ni Ofisa Masoko wa Airtel
Tanzania,Ndevonaeli Eliakimu.
Mpiga Picha wa Magazeti ya Serikali TSN Mohammed Mambo akitafuta picha wakati mkutano huo ukieldelea.
Mpiga picha na mwandishi wa habari wa Chanel Ten Bw. Kibwana Dachi akipata picha katika mkutano huo.
………………………………………………………………………………………………….
Airtel
Tanzania leo imezundia huduma ya kwanza ya kibunifu nchini ijulikanayo
kama “Home WiFi with bundle share” (WiFi ya nyumbani na kufurushi cha
pamoja) itakayowawezesha watanzania na wateja wa Airtel kupata huduma ya
Wi-Fi na kuunganisha zaidi ya vifaa vingine 32 vitakavyotumia WiFi .
Huduma
hii vilevile itaunganisha hadi simu 4 za mkononi zilizoko kokote nchini
kwenye akaunti moja na kuwapatia internet ya kasi ya 3.75G. hii
inamaanisha kifurushi cha internet kilichopo kwenye kifaa cha WiFI ya
nyumbani sasa kitakuwa na matumizi mawili yaani Wifi ya nyumbani na
internet kwenye simu za mkononi pindi mteja akiwa nje ya nyumbani
kwa
sasa wanafamilia na watumiaji wa intenet Tanzania hawana haja ya
kununua vifurushi vya intenet kwa kila simu , kompyuta, Television au
vifaa vyovyote vinavyoweza kuunganishwa na internet na badala yake
watakachotakiwa kufanya ni kununua kifurushi kwenye WiFi ya nyumbani na
kuwawezesha kila aliyeunganishwa na kifaa hicho kupata kifurushi chake
kulingana na gawiwo alilowekea na hivyo kutumia kifurushi kimoja
ili
kujipatia kifaa hichi cha HOME WiFi unaweza ukalipia : shilingi
195,000/- na kupatiwa kifurushi cha kuanzia cha 40 GB kwa mwenzi au
unaweza kulipia shilingi 250,000/- na kupatiwa kifurushi cha kuanzia cha
120 GB kwa mienzi mitatu, Aina zote mbili za ofa zinatoa huduma ya
kutumia kifurushi kimoja na kuunganisha wanafamilia wanne wenye simu za
mkononi ya malipo ya awali (prepaid line)
Akiongea
wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Meneja masoko na bidhaa hii wa
Airtel Bw, Guarav Dhingra alisema” Dunia inabadilika na kukua kwa kasi
ndivyo ilivyo kwa matumizi ya internet, kwa sasa internet si kwa ajili
ya baba na mama, bali ni muhimu kwa familia nzima ikiwa ni pamoja na
watoto kwaajii ya burudani, masomo, na nyingine nyingi. Ongezeko kubwa
la simu za kisasa, komputa ndogo, Television za Kisasa, saa za kisasa,
tablet katika nyumba zetu ni ushahidi tosha wa hili.
Wakati
ongezeko na upatikanaji wa vifaa hivi ukiwa rahisi, njia za
kuunganiswa na huduma za internet zinazidi kuwa ngumu kwa wateja, kwani
inamgharimu mteja kuwa na simcard kwa kila kifaa, na kila simcard
inabidi kusajiliwa na kuwekewa muda wa maongezi wakutosha , kisha
kuingiza namba maalumu na kuchangua kirufushi na ndipo kuanza matumizi.
Airtel
kwa kuona hii changamoto imekuja na huduma ya WiFi ambapo sasa unaweza
kuunganisha vifaa hivi vyote kupitia kifaa cha WiFi cha nyumbani na
kupata intenet ya kasi bila kuhitaji simcard yoyote ya ziada. Na
tumewawezesha wanafamilia kuweza kuongeza kifurushi cha intenet kwa
kupiga *148*20# na kuunganishwa na kifurushi kimoja
Tunaamini
familia nyingi zaidi nchini Tanzania watafurahia na kutumia huduma hii
ya pekee toka Airtel na hivyo kutuamasisha kuongeza huduma nyingi za
kibunifu za internet” aliongeza Guarav Dhingra
Huduma
hii inapatikana kwa kupiga 0784104800 ambapo utaweka oda yako kwajili
ya kupata kifaa hiki cha WiFi ya nyumbani, na kisha Airtel itakuletea
mahali ulipo na kukunganisha na huduma hii.
No comments:
Post a Comment