Na: Dotto Mwaibale
KITUO cha
Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimesema kiwango cha elimu ya haki za
binadamu nchini bado kipo chini hali inayosababisha kukithiri kwa
makundi ya ukatili wa kinjia nchini.
Maandamano yakiingia Makumbusho ya Taifa barabara ya Shabani Robert. |
Maandamano yakiendelea barabara ya Ohio
Wanaharakati Rose Mwalongo na Halord Sungusia wakipeana hi baada ya maandamano hayo kuwasili viwanja vya Makumbusho ya Taifa.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Ezekiel
Masanja akitoa hutuba katika maadhimisho hayo. Kushoto ni Mwenyekiti wa
Bodi ya LHRC, Profesa Geofrey Mmari.
Wawakirishi wa mashirika mbalimbali wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Mwanasheria wa LHRC, Halord Sungusia akitoa mada katika maadhimisho hayo.
Wanakwaya wa Kwaya cha Mwalusanya ambao wapo chini ya LHRC wakitoa burudani za nyimbo za uhamasishaji.
Maofisa wa LHRC wakiwa kwenye maadhimisho hayo. Wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Ujengaji Uwezo na Uwajibikaji, Imelda Urio.
Wadau mbalimbali na wanafunzi wakiwa kwenye
maadhimisho hayo.
Wadau mbalimbali na wanafunzi wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Kufuatia
hali hiyo kituo hicho kinaishauri Serikali kujumuisha elimu ya haki za
binadamu kwenye mfumo wa elimu rasmi inayotolewa nchini ili kupanua
uelewa kwa jamii.
Wanafunzi wakiwa kwenye maadhimisho hayo. |
Hayo
yamesemwa Dar es Salaam leo na Kaimu Mkurungezi Mtendaji wa kituo hicho,
Ezekiel Masanja wakati wa hitimisho la siku kumi na sita za kupinga
ukatili wa kijinsia duniani.
Akitoa
takwimu za nusu mwaka dhidi ya vitendo vya ukatili wa jinsia Masanja
alisema wanawake na wasichana 2878 walibakwa, vilvile vitendo
vilivyoripotiwa polisi nchi nzima ni 3,633.
”Ukatili
upo katika makundi mbalimbali kama vile mauaji ya vikongwe, albino
watoto kubakwa lakini, ukatili, unyanyasaji ambao mara nyingi unafanywa
na ndugu jamaa wa karibu ambao sio rahisi kuwatambua kwa haraka,”
alisema.
Aliongeza
kuwa kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi iliyofanyika mwaka 2012
idadi ya watanzania waliopata elimu rasmi ni zaidi ya milioni 14 kati
yao watu ni zaidi ya milioni 11 wamehitimu elimu ya msigi, wenye elimu
ya chuo kikuu ni zaidi ya laki tatu 3.3.
“Hali hii
inabainisha watu walio na elimu ya dhidi ya haki za binadamu ni
wachache ukilinganisha na mahitaji changamoto inayotokana na mifumo ya
elimu rasmi inayotolewa nchini ,”alisema.
Akizungumzia
kura ya maoni inayotarajiwa kupigwa mwakani alisema wananchi bado
hawana uelewa wa kutosha dhidi ya katiba inayopendekezwa.
“Naiomba
Serikali kutoa mwamko kwa wananchi kwa kusambaza kopi nyingi za rasimu
inayopendekezwa kusudi kuwasaidia wananchi kuelewa nini wanaenda kupigia
kura , “alisema. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)
No comments:
Post a Comment