Sehemu
ya washiriki, ujumbe kutoka Tanzania ukisilikiza ripoti kutoka kwa
mkuugenzi msaidiz idara ya Mazingira ofisi ya makamu wa rais Bw. Richard
Muyungi hayupo pichani kuhusu majadiliano ya mkutano wa dunia wa
badiliko ya tabia nchi unaoendelea mjini Lima Peru.
Katikati waziri wa nchi ofisi ya
makamu wa rais mazingira Dkt Binilith Mhenge,kushoto waziri ofisi ya
makamu wa kwanza wa rais Zanzibar Bi Fatma Fereji kulia Naibu waziri wa
mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Mh Mahadhi Juma Maalim na
sehemu ya washiriki wakifuatilia kuhusu ripoti ya yanayoendelea katika
mkutano wa 20 wa dunia wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiko ya
tabianchi kutoka kwa mkurugenzi msaidizi ofisi ya makamu wa rais
Bw.Richard Muyungi hayupo pichani
……………………………………………………………………………………..
Waziri wanchi Ofisi ya Makamu wa
Rais Mazingira.taaarifa ya namna majadiliano ya mkutano wa 20 wa dunia
wa mabadiliko ya tabia nchi unavyoendela Mjini Lima Peru..
Taarifa hiyo iliyotolewa kwa waheshimiwa mawaziri, waheshimiwa
wabunge, mabalozi makatibu wakuu na wajumbe wa taalam kutoka Tanzania
wanaoshiriki katika mkutano huo wameelezwa kuwa baadhi ya mambo
yanayoendelea kujadiiwa katika mkutano huo ni pamoja na suala la kamati
ya muda ya kisheria kinachoghulikia mkataba mpya wa mabadiliko ya tabia
nchi.
Akiulezea ujumbe huo mkurugenzi msaidizi idara ya mazingira
ambae pia ni mtaalam wa masuala ya tabia nchi bw. Richard Muyungi
amesema kuwa, chombo hiki kimepitia mambo yote muhimu na ya msingi
yanayofaa kuzingatiwa katika makubaliano mapya ambayo yanatarajiwa
kupitishwa mwaka 2015.
Bwana Muyungi aliongeza kuwa jambo lingine linalojadiliwa katika
mkutano unaondelea ni kuhusu masuala ya nchi maskini zaidi
duniani,ambapo ameeleza kuwa mjadala mkuu ulikuwa ni namna ambavyo nchi
hizi maskini zaidi zinavyoweza kufikia misaada ya kifedha kutoka katika
mifuko ya fedha iliyoanzishwa kwenye mkataba wa kimataifa wa mabadiliko
ya tabianchi.
Kwa upande wake mbunge wa Igalula (CCM) Rashidi Mfutakamba
alitaka kufahamu zaidi kuhusu ripoti ya tano ya Dunia ya sayansi kuhusu
mabadilikoya tabia kwa nini haikuhusisha taarifa kamilifu ya athari za
mabadiliko ya tabia nchi kwa watunga sera.
Mbunge Riziki Rulida viti maalum (CCM) alisisitiza umuhimu wa
serikali kuwa na sekretarieti maalum ya kitaifa itakayoshughulia masuala
ya mabadiliko ya tabia nchi pamoja na kutoa elimu kwa umma.
Mheshimiwa waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa kwanza rais
Zanzibar Fatma Fereji alipenda kufaham kuhusu hatua zilizofikiwa
kuhusiana na masuala ya jinsia katika mkataba huo wa kimataifa wa
mabadiliko ya tabia nchi
Awali, waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais mazingira Injinia
Binilith Mahenge alielezea kuhusu uchache wa washiriki kutoka Afrika
katika mikutanao hii ya kimataifa inavyo athiri majadiliano hayo ambapo
tafiti zinaonyesha kuwa nchi zilizoendelea huleta washiriki wa kutosha
na hivyo kuleta mchago mkubwa katika kufanya maamuzi kuhusiana na
mijadala.
Baadhi ya ambao mengine yanayoendela kujadiliwa katika mkutano
huo ni pamoja uharibifu na hasara utokanao na athari zitokanazo na
mabadiliko ya tabia nchi, masuala ya fedha, sayansi na teknolojia,
masuala ya masuala ya upunguzaji gesi joto kupitia sekt ya misitu (
mkuhumi) sera na hatua zinachochuliwa na nchi zilizoendelea katika
kupunga gesi joto.
No comments:
Post a Comment