Na Mwandishi wetu
WACHEZA
tenisi kutoka nchini Kenya wamewafunika watanzania katika michuano ya
kimataifa ya kwanza ya tenisi kwa walemavu (Dar Open ).
Michuano hiyo inatarajiwa kuhitimishwa kesho katika viwanja vya Gymkhana, majira ya saa 10 ambapo washindi watapewa tuzo zao.
Kwa
mujibu wa matokeo ya hadi mchana wakati mwandishi wa habari hizi
anaondoka viwanjani hapo, mechi saba zilienda kwa wakenya kwa nafasi ya
wanaume na wanawake na mbili ndio walishinda Watanzania.
Michuano
hiyo ambayo inadhaminiwa na kampuni ya magari ya CFAO, Mercedes-Benz na
kampuni ya mawakili ya Dar es salaam ya IMMMA imelenga pia kuandaa
wachezaji kwa ajili ya mechi za kufuzu michezo ya dunia zinazotarajiwa
kupigwa nchini Kenya Februari mwakani.
Kwa
mujibu wa msemaji wa wadhamini wa michuano hiyo Alexander Sarac,
michuano hiyo yenye washiriki wanaume 17 na wanawake watano walioitwa
kutoka Tanzania na Kenya, imelenga kuwezesha walemavu kuendeleza vipaji
vyao vya kucheza tenisi.
Pamoja
na kuwa na ushindi dhaifu wa watanzania kocha wa timu ya Tanzania
amesema bado ana bunduki zake mbili na ana hakika kesho vikombe vitabaki
Tanzania.
Fungua
dimba ya michuano hiyo ilianzishwa na watanzania Novatus Temba na Moses
Sebastian ambapo Temba alimchapa Sebastian kwa seti 2-0; mkenya Itaken
Timoi alimvuruga Bernad Antony kwa seti 2-0 huku Mkenya mwingine Peter
Mnuve akimtoa Mtanzania Albert John kwa seti 2-0.
Muingereza anayeishi nchini Ian Artetiel alimtoa Mtanzania Voster Peter kwa seti 2-1.
Mkenya
Caleb Odisyo alimchapa Mtanzania Wiston Sango kwa seti 2-0 wakati
katika mechi za wanawake, Mtanzania Rehema Seleman alimsulubu bila
huruma Asia Mohamed wa Kenya seti 2-0.Katika mechi nyingine Asia Mohamed
alimchapa Bihawa Mustafa kwa seti 2-1.
Naye Lucy Shirima wa Tanzania alitandikwa na Phoebe Masika wa Kenya kwa seti 2-0.
Timu
ya Tanzania ambayo kwa sasa ndiyo inayotamba Afrika Mashariki kutokana
na michuano ya mwisho iliyofanyika Nairobiu kutwaa ushindi ina kazi ya
ziada kulinda heshima yake.
No comments:
Post a Comment