Katika mtaa,mdogo wa Shanghai, kilichokuwa kiwanda cha kushona nguo sasa kimegeuka, ishara ya mabadiliko ya kuchumi yanayoshuhudiwa nchini China.
Katika eneo hili, wafanyakazi walikuwa wanafanya kazi ndogondogo kujikimu kimaisha na hata kuuza bidhaa zao nje , lakini kazi mpya imeanza kufanyika hapa.
Biashara hii ni moja ya biashara ambazo zinasukuma uchumi wa China kwa kuwafanya watu kutumia pesa zao.
Duka lililofunguliwa hapa linaitwa Mr Wedding ...Biashara ndogo ambayo inawaajiri watu 16 ni sehemu ya sekta ambayo imekuwa ikinawiri kuliko nyinginezo katika historia ya nchi hii.
Kulingana na taarifa za serikali, soko la biashara za bidhaa za harusi , pesa zinazotumika kwa sherehe aina zote za harusi imekuwa kwa kasi na kuwa na thamani ya dola bilioni 130 kila mwaka.
Duka hili la Mr Wedding halijaachwa nyuma kwani nalo linataka kipande cha mapato kutoka kwa sekta hiyo. Tofauti ya biashara yake ni kwamba maharushi hupata huduma ya kipekee kutoka kwa duka lake.
'Mtindo tofauti wa Picha'
''Watu wanaweza kupigwa picha ndani maji wakiwa katika hali yoyote, '' asema mmiliki wa duka hili Tina Liu.
"maharusi huonekana wakielea ndani ya maji, na picha hizi huwapendeza wengi sana. ''
|
No comments:
Post a Comment