Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mh. Peter Kalaghe akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Bodi ya Utalii Kushoto ni
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bi. Devotha
Mdachi na kutoka kushoto ni Meneja wa Masoko wa (TTB) Bw. Geofrey Meena
na Mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bi.
Teddy Mapunda
Balozi
wa Tanzania nchini Uingereza Mh. Peter Kalaghe na Garry Hutchinson
Mkurugenzi wa Biashara wa timu ya ligi kuu ya Uongereza ya Sunderland
wakionyesha jezi ya iliyoandikwa Tanzania yenye rangi za timu hiyo
wakati wa uzinduzi rasmi wa matangazo ya Utalii wa Tanzania
yanayotangazwa katika uwanja wa timu hiyo huko Sunderland Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mh. Peter Kalaghe katikati akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Bodi ya Utalii kutoka kulia Meneja wa Masoko wa (TTB) Bw. Geofrey Meena,
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bi. Devotha
Mdachi na kutoka kushoto ni Mdau wa Utalii Bw. Nesto Mapunda na Mjumbe
wa Bodi ya wakurugenzi ya Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bi. Teddy
Mapunda Wachezaji
wa timu ya Sunderland wakipasha mwili huku wakiwa wamevalia fulana
nyeusi zenye maandishi yanayotangaza na kukaribisha watalii na kutangaza
utalii nchini Tanzania. Matangazo yakiendelea kuonyeshwa kwenye mbao za matangazo wakati mchezo kati ya Chealsea na Sunderland ukiendelea. Fulana zinazotangazo utalii wa Tanzania ikiwa zimewekwa kwenye vyumba vya kubadilishia jezi wachezaji wa timu ya Sunderland. Majarida
yanayotangaza utalii wa Tanzania yakiwa yamesambazwa kwenye meza katika
mgahawa wa timu ya Sunderland kwenye uwanja wao wa Sunderland Mabango na yanayotangaza utalii wa Tanzania yakiwa yamewekwa kwenye makumbusho ya timu hiyo. Haya ni baadhi ya mabango yanayoonyeshwa katika uwanja huo wakati wa michezo ya Ligi kuu. Bendera
yenye maandishi ya kukaribisha watalii kutembelea Tanzania ikiwa
imepandishwa katika miliongoti katika lango kuu la uwanja huo.
………………………………………………………………………………………………
Bodi
ya Utalii Tanzania (TTB) imeshirikiana na Timu ya mpira wa miguu ya
Sunderland (SAFC) ya nchini Uingereza katika uzinduzi wa utangazaji
utalii wa Tanzania pamoja na kuhamasisha uwekezaji kwenye sekta ya
michezo (Destination Partner in Tourism and Sports Development).
Uzinduzi huo ulifanyika tarehe 29 Novemba, 2014 kwenye kiwanja
kinachomilikiwa na timu ya Sunderland “Stadium of Light”
Kwenye
tukio hilo ambalo lilihudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza,
Mheshimiwa Balozi Peter Kallaghe pamoja na, maafisa kutoka Bodi ya
Utalii, Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza pamoja na watanzania
waishio nchini Uingereza. Tukio hili lilifanyika wakati timu ya Mpira ya
Sunderland ilipoikaribisha timu ya mpira ya Chelasea Football club.
Wakati
wa uzinduzi huo matangazo ya Utalii yaliweza kurushwa katika kingo za
kuta za uwanja wa timu ya Sunderland na kuonesha vivutio vya vivutio vya
utalii wa Tanzania na vile vile yalioneshwa kwenye luniga kubwa
iliyokuwepo kwenye uwajani huo. Aidha wachezaji wa timu ya Sunderland
walivaa jezi maalum zilizoandikwa ‘Visit Tanzania’ wakati wakifanya
mazoezi mepesi kabla ya mechi kuanza.
Bodi
ya Utalii Tanzania ilitumia fursa ya uziduzi huu kuhamasisha wataliii
kutoka ndani na nje ya Uingereza pamoja na mashabiki wa timu hizo
kutembelea vivutio vya utalii wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment