Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kulia) akipokea
msaada wa vifaa mbalimbali vya kuzima moto pamoja na makoti ya kujikinga
na kemikali, kutoka kwa Balozi wa Uingereza nchini, Dianna Melrose
(kulia). Msaada wa vifaa hivyo ambavyo tayari vimeingia nchini kwenye
kontena maalumu pia kuna kofia ngumu kwa ajili ya Jeshi la Polisi,
pamoja na aina mbalimbali ya mabuti jeshi, suruali maalumu kwa ajili ya
kupambana katika matukio mbalimbali na viatu vya kiume na kike. Kushoto
ni Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Paulo Chagonja
na Kaimu Kamishna Operesheneni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Christom
Manyologa ambao walikabidhiwa vifaa hivyo baada ya kupokelewa na Waziri
Chikawe katika ukumbi wa wizara hiyo.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia) akimshukuru Balozi
wa Uingereza nchini, Dianna Melrose kwa msaada wa vifaa mbalimbali vya
kuzima moto pamoja na makoti ya kujikinga na kemikali ambayo vifaa hivyo
vimetolewa kwa ajili ya Jeshi la Polisi na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
ili kukabiliana na matukio mbalimbali nchini. Picha zote na Felix
Mwagara Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment