WAZIRI wa Kazi na Ajira nchini
Tanzania, Gaudensia Kabaka ameipongeza Benki ya Posta Tanzania (TPB)
pamoja na Mfuko wa PSPF kwa kushirikiana na kuanzisha mpango wa utoaji
wa mikopo ya elimu kwa vijana pamoja na mkopo wa kuanzia maisha kwa
wafanyakazi. Waziri Kabaka ametoa pongezi hizo leo jijini Dar es Salaam
alipokuwa akizinduwa huduma ya mkopo wa elimu kwa wanachama wa mfuko wa
PSPF iliyofanyika katika Ukumbi wa Golden Jubelee Tower.
Alisema huduma za mikopo ya elimu
na kuanzia maisha ni huduma muhimu sana kwa vijana kwani upataji wa
fedha za kujiendeleza kwa kundi hili imekuwa changamoto kubwa hivyo
kupatikana kwake itafungua milango kwa vijana kujiendeleza kielimu bila
vikwazo.
Akizungumzia huduma ya mkopo wa wa
kuanzia maisha alisema huduma hiyo imekuja wakati muafaka kwani mtu
anapoanza kazi anakuwa akihitaji vitu muhimu na vya msingi katika maisha
lakini wamekuwa wakikwamishwa na hali ya kipato. Hivyo mkopo huu
utakuwa mkombozi wa wengi wanaoanza maisha kazini.
“…Kitu kilichonifurahisha zaidi ni
jinsi PSPF mlivyoshirikiana na Benki ya Posta Tanzania katika kubuni,
kupanga, kuandaa na hatimaye kutekeleza utaratibu huu, hili ni jambo
sahihi na muafaka kwani kwa mujibu wa taratibu za Mifuko ya Hifadhi ya
Jamii duniani kote kazi za mifuko hii sio kutoa mikopo bali ni
kuwawezesha wanachama wake kupata mafao yao stahili pale wanapostaafu,”
alisema Waziri Kabaka.
|
Waziri
wa Kazi na Ajira nchini Tanzania, Gaudensia Kabaka akizungumza katika
uzinduzi wa huduma ya mikopo ya elimu na kuanzia maisha kwa wanachama wa
Mfuko wa PSPF jijini Dar es Salaam. Huduma hiyo inatekelezwa kwa
ushirikiano na Benki ya Posta Tanzania (TPB) na Mfuko wa PSPF. |
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, Sabasaba Moshingi
akizungumzia katika hafla ya uzinduzi wa huduma ya mkopo wa elimu kwa
wanachama wa mfuko wa PSPF leo jiji ni Dar es Salaam.
Waziri
wa Kazi na Ajira nchini Tanzania, Gaudensia Kabaka akizinduwa huduma ya
mikopo ya elimu na kuanzia maisha kwa wanachama wa Mfuko wa PSPF jijini
Dar es Salaam.
Ofisa Mtendaji Mkuu, PSPF Adam Mayingu akizungumza katika uzinduzi huo.
|
Waziri
wa Kazi na Ajira nchini Tanzania, Gaudensia Kabaka akiwasili katika
Ukumbi wa Golden Jubelee Tower pamoja na viongozi wakuu wa Benki ya
Posta Tanzania na Mfuko wa PSPF tayari kwa uzinduzi wa huduma ya mikopo
ya elimu na kuanzia maisha kwa wanachama wa Mfuko wa PSPF jijini Dar es
Salaam. |
|
Waziri
wa Kazi na Ajira nchini Tanzania, Gaudensia Kabaka akizinduwa huduma ya
mikopo ya elimu na kuanzia maisha kwa wanachama wa Mfuko wa PSPF jijini
Dar es Salaam. |
Waziri
wa Kazi na Ajira nchini Tanzania, Gaudensia Kabaka akiwa amewanyanyua
juu mikono Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, Sabasaba
Moshingi (kushoto) na Ofisa Mtendaji Mkuu, PSPF Adam Mayingu (wa pili
kulia) mara baada ya uzinduzi wa huduma ya mikopo ya elimu na kuanzia
maisha kwa wanachama wa Mfuko wa PSPF jijini Dar es Salaam.
Kutoka
kushoto ni Waziri wa Kazi na Ajira nchini Tanzania, Gaudensia Kabaka,
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, Sabasaba Moshingi na
viongozi wengine wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa huduma ya mikopo ya
elimu ya juu kwa vijana.
Balozi wa Mfuko wa PSPF, Mrisho Mpoto (mjomba) akiwa katika hafla hiyo ya uzinduzi.
Uzinduzi wa huduma ya mikopo ya elimu na kuanzia maisha kwa wanachama wa Mfuko wa PSPF jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Posta Tanzania na PSPF wakiwa katika uzinduzi huo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Posta Tanzania na PSPF wakiwa katika uzinduzi huo.
Akizungumza katika hafla ya
uzinduzi wa mpango huo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania,
Sabasaba Moshingi alisema TPB inatambua mzigo mkubwa uliobebwa na
Serikali katika kuwasomesha vijana hivyo imeamua kubeba jukumu la
kuwasaidia vijana kukopa kwa lengo la kujiendelea kielimu.
“Benki ya Posta inatambua mzigo
mkubwa uliobebwa na Serikali katika kuwasomesha vijana wetu katika vyuo
vikuu mbalimbali hapa nchini, na tukiwa kama Benki halisi ya Kitanzania
tumeamua kwa dhati kabisa kuisaidia Serikali katika nyanja hii,
tukishirikiana na wenzetu wa PSPF,” alisema Moshingi.
Alisema hata hivyo Benki ya Posta
imeendelea kubuni huduma za kibenki mbalimbali kwa ajili ya kukidhi
mahitaji ya wananchi wa kila kada hapa nchini. Alisema Mwezi Machi 2014
benki hiyo iliingiza huduma mpya ya mikopo kwa kundi la wastaafu nchini
jambo ambalo limekuwa faraja kubwa kwa wastaafu nchini.
“…Adhma yetu ni kuhakikisha kuwa
tunamkomboa kiuchumi mwananchi, hususan mwenye kipato cha chini kwa
kumpatia mkopo wenye riba nafuu. Mkopo huu wa elimu uliozinduliwa leo
una lengo la kumsaidia mwanachama wa PSPF kutimiza ndoto zake kwa
kujiendeleza kielimu katika ngazi yoyote, stashahada, shahada, shahada
ya uzamili na nyinginezo,” alisema.
“Mwanachama wa PSPF anayetaka
kukopa aina hii ya mkopo atadhaminiwa na mwajiri wake, pia mkopo huu
unabima, hivyo endapo mkopaji atafariki familia yake haitaendelea
kudaiwa na riba inayotozwa kwa mkopo huu ni nafuu yaani asilimia 14 tu
kwa mwaka,” alisisitiza Moshingi.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com
No comments:
Post a Comment